MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

LightBlog

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, March 1, 2018

Dk Shein awaapisha mawaziri, wakuu wa wilaya

3:00:00 AM 0
 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein leo Machi 1, 2018 amewaapisha viongozi aliowateua jana Februari 28, 2018 kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ).
Taarifa iliyotolewa na Ikulu Zanzibar leo, inaeleza kuwa hafla hiyo imefanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali.
Baadhi ya viongozi hao ni Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd; Spika wa Baraza la Wawakilishi,  Zubeir Ali Maulid; Jaji Mkuu wa Zanzibar, Omar Othman Makungu; Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar,  Said Hassan Said; mawaziri, naibu mawaziri na wakuu wa mikoa.
Walioapishwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi, Amina Salum Ali;  Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Ali Abeid Karume; Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji na Dk Sira Ubwa Mamboya.
Wengine ni Waziri wa Afya, Hamad Rashid Mohamed; Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi,  Rashid Ali Juma; Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Salama Aboud Talib; Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Mahmoud Thabit Kombo pamoja Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto, Maudline Cyrus Castico.
Pia wamo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Juma Makungu Juma;  Naibu Waziri wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Choum Kombo Khamis; Naibu Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto, Shadia Mohamed Suleiman; Naibu Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Dk Makame Ali Ussi na  Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda, Hassan Khamis Hafidh.
Pia, Dk. Shein amewaapisha wakuu wa wilaya aliowateua ambao ni  Issa Juma Ali (Mkoani-Pemba) na Rajab Ali Rajab wa Kaskazini B, Unguja.
Viongozi walioapishwa wameahidi kuendelea kumsaidia Rais Dk. Shein katika kuhakikisha Zanzibar inazidi kupata maendeleo, kuimarisha ushirikiano na kuwatumikia wananchi.
Pia, wameahidi kuleta mabadiliko na kufanya kazi kwa vitendo sambamba na kuendelea kusimamia amani na utulivu uliopo nchini.
Jana, Dk Shein alifanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mapinduzi kwa kuongeza wizara moja zaidi na kuwabadilisha wizara baadhi ya Mawaziri.
Kufuatia mabadiliko hayo, shughuli za vijana zimehamishiwa katika Wizara mpya ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo shughuli za mazingira zimehamishiwa katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais na shughuli za Wakala wa Serikali wa Uchapaji zimehamishiwa Wizara mpya ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale.
Aidha, amewateua naibu mawaziri wapya wawili na kumbadilisha wizara naibu waziri mmoja ambapo kufuatia mabadiliko hayo, SMZ hivi sasa ina wizara 14.
Read More

Simba, Yanga FC zachibwa mkwara na KARIA

2:44:00 AM 0
 
 
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ametamka kuwa hataruhusu klabu yoyote kucheza Ligi Kuu Bara kama itakuwa haijawakatia bima wachezaji wake watakaowatumia katika msimu wa 2018/2019.
 
Kauli hiyo, aliitoa kwenye ufunguzi wa semina ya utawala bora kwa klabu za ligi kuu na Ligi Daraja la Kwanza iliyofanyika jana Rombo Green View iliyokuwepo Ubungo jijini Dar es Salaam ambayo ilihusisha klabu kongwe za Simba na Yanga.
 
Semina hiyo, iliandaliwa na Kampuni ya Maendeleo na Utafiti wa Michezo (ISDI) kwa kushirikiana na Alliance Life Assuarance na TFF kwa lengo la kutoa elimu kwa viongozi wa klabu kujua jinsi ya utawala, kujiongoza na kutafuta wadhamini.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari kabla ya kufungua semina hiyo, Karia alisema kikubwa anataka kuona klabu maendeleo na mafanikio kwa klabu hizo huku akiamini kupitia semina hiyo wawakirishi hao watapata elimu nzuri.
 
 
Karia alisema, moja ya maendeleo anayotaka kuyaona ni klabu kuwakatia bima wachezaji wake ambalo amepanga kulisimamia mwenyewe na hataruhusu timu yoyote kucheza ligi kama itakuwa haijakamilisha zoezi hilo.
 
“Niseme kuwa, sitakuwa na masihala juu la hili la bima ni lazima kila klabu iwakatie bima ya afya wachezaji wake na uzuri wapo hapa Alliance Life Assuarance ambao wanausika na bima, hivyo tutazungumza nao kujua jinsi ya kufanya.
 
“Niseme kuwa, kama klabu haitakuwa imewakatia bima wachezaji wake, basi haitacheza ligi kuu msimu ujao na hilo nitahakikisha ninalisimamia vizuri na kama itakuwepo klabu imeshindwa kutimiza hilo basi itatakiwa kuwasiliana na bodi ya ligi tujue jinsi ya kuwasaidia ili wakatiwe bima,”alisisitiza Karia.
 
“Na hilo alitaangalia ukubwa wala udogo wa klabu ni lazima kila timu ifuate kanuni za ligi kuu ambazo tumeziweka,”alisema Karia.
 
SOURCE: global publisher
Read More

Tuesday, January 30, 2018

LIVE VIDEO: JPM Azindua Hati za Kusafiria

10:42:00 PM 0
Tazama hapa chini Video Rais John Magufuli Akizindua hati za kusafiria.


Read More

Saturday, January 27, 2018

Aslay akemea mashabiki kumfananisha na Rich Mavoko

3:50:00 AM 0
Msanii wa muziki Bongo, Aslay amesema si vizuri kufananishwa na Rich Mavoko kwani ni msanii ambaye amemtangulia katika muziki.
Muimbaji huyo amesema Rich Mavoko amekuwa akifanya vizuri kila siku, hivyo mashabiki wanaomshindanisha wanakosea.
“Huwezi kunishindanisha na Rich Mavoko, yule ni kaka yangu halafa anafanya vitu vikubwa, nimemkuta kwenye muziki na amefanya vitu vikubwa, kwa ukisema unanishindanisha na Rich Mavoko utakuwa unakosea,” Aslay ameiambia Bongo5.
Katika hatua nyingine Aslay ameeleza sababu ya yeye kuwa miongoni mwa wasanii ambao ngoma zao zinapata views zaidi katika mtandao wa YouTube.
“Ni mashabiki wangu wa kweli ndio maana unakuta hata nikitia ngoma leo kesho unakuta nina laki moja, kwa hiyo siwezi kusema labda nilikuwa nashindana au nina vitu vikubwa sana navifanya niwe na views wengi YouTube ni mashabiki zangu kunipenda kweli,” amesema.
Read More

VIDEO: Pah One - Hatuna Hbari

3:28:00 AM 0
Kundi la Pah One wamerudi kivingine baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu, wameachia video ya ngoma yao mpya ‘Hatuna Habari’, video imeongozwa na Mims. Itazame hapa.


Read More

Vifahamu Vyakula Vinavyoondoa Mumivu ya Hedhi

3:19:00 AM 0

Kila mwanamke hupitia hatua ya kupatwa na hedhi mara moja kwa mwezi, ikiwa ni maumbile ya kawaida waliyoumbwa nayo. Lakini wanawake wengi husumbuliwa na matatizo kadhaa siku chache kabla au wakati wa siku zao, matatizo hayo hutofautiana kati ya mtu na mtu kutegemeana na afya ya muhusika, wapo baadhi ya wanawake huumwa na kiuno, wengine tumbo n.k

Dlili za matatitizo ya hedhi
Siku chache kabla ya hedhi, baadhi ya wanawake hupatwa na hofu na huwa wenye hasira. Husumbuliwa na mfadhaiko wa akili, huumwa na kichwa, matiti hujaa maziwa, hukosa usingizi na kuvimba sehemu za siri. Hali hii husababishwa na kukosekana kwa uwiano wa homoni (Homone imbalance) na hali hii huweza kukoma ndani ya saa 24 baada ya kuanza hedhi.

Wengine hupatwa na maumivu makali sana wakati wa hedhi. Maumivu hayo huwapata akina mama ama siku mbili ama tatu kabla au mara tu waanzapo siku zao. Hali hii pia inasababishwa na kutokuwepo kwa uwiano wa homoni mwilini, ambako kumesababishwa na ukosefu wa virutubisho fulani.

Wengine hutokwa na damu nyingi kuliko kawaida au kukaa katika siku za hedhi kwa kipindi kirefu kuliko kawaida. Kuna sababu nyingi zinazoweza kuchangia hali hii, ikiwemo kuugua kwa muda mrefu, kupatwa na hofu, huzuni, mshtuko na sababu nyingine za kitabibu.

Vifatatavyo ni vyakula vinavyoweza kutibu maumivu wakati wa hedhi

2. Tangawizi
Tangawizi nayo ni dawa nzuri sana ya kutibu matatizo yatokanayo na hedhi, hasa katika tatizo la maumivu makali na kutokupata hedhi. Chukua kipande cha tangawizi mbichi, kiponde na kiweke kwenye kikombe cha maji ya moto kwa dakika chache, kisha tia sukari kiasi na unywe mchanganyiko huo, kwa siku mara mbili kila baada ya mlo.

2. ufuta.
Ufuta (Sesame) nao ni miongoni mwa mbegu za asili unazoweza kula na kutibu matatizo ya hedhi. Saga ufuta na pata unga wake kisha uchanganye na maji ya moto, kunywa mara mbili kwa siku. Kinywaji hiki huondoa maumivu wakati wa hedhi kwa wasichana wadogo.

Ukitumia mara kwa mara kinywaji hiki cha ufuta, hutibu pia tatizo la kupata hedhi kidogo. Pia unaweza kuchangaya maji ya kuoga ya uvuguvugu na mbegu za ufuta zilizopondwa pondwa kiasi cha kiganja kimoja, nayo hutoa nafuu kubwa kwa wanaosumbuliwa na maumivu, hasa ukitumia siku mbili kabla ya siku zako.

3. Papai
Mungu ametuumba na kutupa mazao mengi ambayo yana uwezo wa kutatua matatizo yetu ya kiafya, iwapo tutagundua siri hiyo. Papai bichi nalo linaelezwa na watafiti wetu kuwa lina uwezo wa kulainisha misuli ya njia ya uzazi hivyo kufanya utokaji wa hedhi kuwa mwepesi usio na maumivu. Papai huwa na manufaa zaidi kwa wasichana haswa kwa wale wenye tatizo la kutopata siku zao kutokana na kuwa na ‘stress’ au mawazo. Utapata faida hiyo kwa kula mara kwa mara tunda hilo bichi (ambalo halijaiva lakini limekomaa)

4. Juisi za mboga za majani.
Kwa kutumia vyakula asilia unaweza kuepukana na maumivu ya mara kwa mara wakati wa siku zako. Katika orodha ndefu ya juisi za mboga zinazotibu kwa uhakika matatizo yote ya hedhi, ni Kotimiri (Parsley), mboga ya majani ambayo upatikanaji wake ni rahisi. Kwa mujibu wa watafiti, Kotimiri ina uwezo wa kurekebisha uwiano wa homoni hivyo kuondoa matatizo kadhaa ya hedhi.

Inaelezwa kuwa uwezo wa Kotimiri kurekebisha matatizo ya hedhi unatokana na kuwa na aina ya kirutubisho kiitwacho ‘Apiol’ ambacho pia kimo miongoni mwa homoni za jinsia ya kike (estrogen). Maumivu na mvurugiko wa siku hurejea katika hali ya kawaida kwa kunywa juisi ya Kotimiri mara kwa mara.

Aidha, juisi hiyo inapochanganywa na juisi ya viazi pori (Beet Root), karoti au matango huwa na nguvu zaidi. Kiwango kinachoshauriwa kuchanganya kiwe na ujazo sawa kwa kila aina ya juisi utakayochanganya. Juisi yenye mchanganyiko huo ni rahisi kutengeneza na ni dawa inayoweza kumsaidia mwanamke wakati wote wa maisha yake bila kuhitaji kutumia dawa zingine kali za kuzuia maumivu (pain killers) ambazo huwa na madhara baadaye
Read More

Ruby, Clouds Media Bifu limekwisha

2:53:00 AM 0

Msanii wa muziki Bongo, Ruby amemaliza tofauti baina yake na Clouds Media Group. 

Muimbaji huyo ametumia kipindi cha XXL kuwaomba radhi wale wote aliowakwaza katika chombo hicho cha habari.

“Yeyote, awe ni mwanakamati wa Clouds, team Clouds au awe ni shabiki wa nje I like to apologize guy to say sorry to my country, sorry to this management Clouds, I love them so much all I need is support mimi naamini kwamba ukiwa mjinga kwenye kila kitu utapata kujua vitu vingi sana,”
amesema Ruby.

“Nilikaa nikamuomba Boss wangu Ruge samahani, mimi ni mdogo wewe ni mkubwa, of course kwa chochote kile mimi ndio nakosea,” amesema.

Clouds Media Group walikuwa wamesitisha kucheza nyimbo za msanii huyo kutokana na tofauti zao, hivyo sasa nyimbo zake zinachezwa na inaelezwa tangu November mwaka jana ilitolewa ruhusu kwa ngoma zake kuchezwa.
Read More

BREAKING NEWS: IGP Sirro azungumza na Viongozi wa Dini

Trump, Kagame Uso kwa uso

12:43:00 AM 0

Rais wa Marekani, Donald Trump amekutana na kufanya mazungumzo na Paul Kagame ambaye ni Rais wa Rwanda na  Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) na kumuomba afikishe salamu zake za upendo kwa viongozi wengine wa mataifa wanachama wa AU.

Viongozi hao wawili wamekutana mjini Davos, Uswizi baada ya Mkutano wa Viongozi na Watu Mashuhuri Kuhusu Uchumi na Biashara Duniani, Mkutano huo wa Kagame na Trump umekuja wiki chache baada ya kiongozi huyo wa Marekani kutoa kauli iliyotafsiliwa kama ni kuyakashifu mataifa ya Afrika.

Hatua hiyo ilimfanya kushutumiwa vikali na viongozi wa AU na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika kama vile Botswana na Ghana ambapo amekanusha kwamba alitumia neno hilo kuyakashifu mataifa ya Afrika huku akikiri kutumia maneno makali akiyaeleza mataifa ya Afrika, Haiti na El Salvador alipokuwa anazungumzia wahamiaji wanaoingia Marekani.

Wakati wa mkutano wake na Kagame,  Trump hajaonyesha dalili zozote za majuto kuhusu tamko lake la awali kuhusu Afrika huku akisifia kuwa mkutano wao huo ulikuwa “wa kufana sana”, na kueleza nchi hizo mbili kama washirika wa kibiashara ambao wanajivunia “uhusiano mzuri sana.”

“Ningependa kukupongeza, Bw Rais, unapochukua majukumu ya kuwa kiongozi mpya wa Umoja wa Afrika, ni heshima kubwa … najua unaenda kuhudhuria mkutano wa kwanza karibuni. Tafadhali, fikisha salamu zangu.”

Rais Kagame alisema wameshauriana kuhusu ushirikiano wa nchi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na usaidizi wa Marekani kwa Rwanda katika operesheni zake kote duniani, pamoja na masuala ya kiuchumi, biashara, uwekezaji na idadi ya watalii wa Marekani wanaozuru Rwanda, ambayo inaongezeka. Mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa AU utafanyika kesho Jumapili na Jumatatu.
Read More

Thursday, January 25, 2018

Mke Kumtaka wema aolewe na Nabii Tito

1:27:00 AM 0
African Sweetheart, Wema Sepetu
 Katika hali isiyotarajiwa, imeelezwa kuwa msanii nyota wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, amemlipua mke wa ‘Nabii’ Tito baada ya mwanamke huyo kumshawishi kupitia mitandaoni aolewe na nabii huyo.

Chanzo makini kilisema kuwa, msanii huyo amekasirishwa na kitendo cha mke huyo kumshawishi kuolewa na mumewe anayeitwa Onesmo Machija ‘Nabii Tito’ (44).

“Wema Sepetu nakupenda sana hata Nabii Tito anakupenda sana, kwanza mzuri, una shepu nzuri hata katika mambo ya Kiafrika unaongoza kwa uzuri.

“Nabii Tito huyo kwa watu wasiomfahamu wanasema sio nabii lakini kwa mimi ninayemfahamu na kuishi naye naona mambo ya kinabii anayofanya, nakuomba ukubali hata mimi nakupenda sana, kwanza una shepu nzuri.

“Uwe mke mwenzangu, ukubali kuwa mke wa Nabii Tito. Sikia kilio cha mke wa nabii,” amesikika kwenye video mke huyo wa Nabii Tito akimbembeleza Wema.

Naye Nabii Tito kwenye video hiyohiyo amechombeza kwa kubembeleza kwamba Wema akubali kuwa mkewe ili kanisa lao likuwe.

Alipotafutwa Wema na kuulizwa kuhusiana na video hiyo alisema, ameiona na amekasirishwa na kile walichokifanya nabii huyo na mkewe.

“Kiukweli wameniudhi sana kwa kunidhalilisha. Nawasiliana na mwanasheria wangu ili nimburuze mahakamani mwanamke huyo,” alisema Wema.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi mkoani Dodoma, mapema wiki hii lilimkamata nabii huyo na kumfanyia mahojiano kutokana na mahubiri ya kidini anayoyafanya na limesema mtu huyo ana matatizo ya akili.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, SACP Gillesi Muroto amesema Juni 23, 2014, mtu huyo aliwahi kulazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya matibabu ya akili chini ya daktari aliyejulikana kwa jina moja la Dk. William ambapo aliporuhusiwa alitakiwa kurejea hospitalini hapo Julai 9 mwaka huohuo lakini hakurejea.

Kamanda Muroto aliendelea kusema kwamba, baada ya hapo Machija ambaye kanisa lake halijasajiliwa popote, aliibukia mkoani Dodoma katika Kijiji cha Nong’ona kilicho karibu na Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) akifanya mahubiri ya kidini yaliyodaiwa kuwa hayakuwa na maadili ya kidini.

“Kwa msingi huo, jeshi la polisi limempeleka Hospitali ya Rufaa ya Milembe iliyoko mkoani Dodoma kwa ajili ya kumpima tena matatizo hayo ya akili na baada ya majibu kutolewa, Dk. Dixon Philipo aliyemshughulikia alithibitisha kwamba bado ana matatizo hayo ya akili,” alisema kamanda Muroto juzi na kusisitiza kuwa wanaendelea kumshikilia kutokana na matendo yake aliyoyafanya ili kufanya uchunguzi zaidi.


Nabii Tito na mkewe pamoja na mfanyakazi wake wa ndani.
Read More

Post Top Ad

Your Ad Spot