Na Penina Malundo
WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma Shule ya Msingi Kivule iliyopo Kata ya Kivule wilayani Ilala jijini Dar es Salaam, wamemkataa Mwenyekiti wa Kamati ya Shule, Dustani Tadeo aliyechaguliwa juzi kwa madai kuwa aliwahi kutumia vibaya fedha za kanisa. Hatua hiyo inatokana na wazazi kutoridhishwa baada ya msimamimzi wa uchanguzi huo kumtaja, Tadeo kuwa ndiye Mwenyekiti wa shule hiyo. Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano huo shuleni hapo, wazazi hao walidai hawamtaki, Tadeo kutokana na kudaiwa kutumia vibaya fedha za kanisa. Mmoja wa wazazi waliohudhuria kikao hicho Jackson Paul alidai, wana wasiwasi shule hiyo ikakosa maendeleo endapo Tadeo atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya shule. “Tadeo hataifikisha shule mahali pa zuri kutokana na kutuhumiwa na uongozi wa kanisa fulani lililopo Ukonga kuwa alitumia vibaya fedha za kanisa hilo hivyo tunaona hapa napo atatumia vibaya tu maana kama alishindwa kumwogopa Mungu akala ela zake, Je kwetu atashindwa vipi kuzitumia? ili ni jipu lazima litumbuliwe kabla halijaanza kuumiza watu wengine," alidai. Akijibu tuhuma hizo, Tadeo alisema ni kweli alishawahi kutunza fedha za Kanisa la Katoliki la Ukonga na baadaye alihamia Kanisa la Kitunda. “Ni kweli niliwahi kutunza fedha za kanisa lakini sikula fedha yoyote na kama hawaamini wakamuulize Paroko na nilihamia katika Kanisa la Kitunda hivyo tuhuma hizo mnazozisema hata sijui mmezitoa wapi maana mi mwenyewe hata sitambui hicho mnachokisema,” alisema. Naye ambaye ni mmoja wa wazazi hao, Hadija Mwinyimua alisema katika kipindi cha uongozi wa Mwenyekiti wa shule hiyo, Bihimba Mpaya aliyemaliza muda wake aliweza kusimamia mambo mengi ya maendeleo ya shule na kwamba bado wana imani naye. “Mpaya alisema ukweli ndiyo maana hawakumchagua ameweza kusimamia, kupiga marufuku biashara shuleni hapa ambapo awali watoto wetu walikuwa wakilazimishwa kununua ‘Ice crem’ambazo zilikuwa si salama kutokana na mazingira yanayotengenezwa ,”alisema Kutokana na wazazi hao kumkataa mwenyekiti huyo na kulundikana katika mlango wa moja ya chumba walipokaa uongozi huo mpya Diwani wa Kata hiyo Wilson Mollel alimwomba msimamizi wa uchaguzi huo Julius Maembe kuiacha nafasi hiyo wazi mpaka watakapopata maelekezo kutoka ngazi ya juu.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Saturday, August 6, 2016
WAZAZI wa wanafunzi wamemkataa kwa kutumia vibaya fedha
Tags
# KITAIFA
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot


No comments:
Post a Comment