MASWALI 5 KATI YA 10 YA KUJIULIZA KWA WATU WALIO KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 21, 2016

MASWALI 5 KATI YA 10 YA KUJIULIZA KWA WATU WALIO KATIKA MAHUSIANO YA KIMAPENZI


Moja kati ya watu waliopo kwenye mapenzi.
UNAPOKUWA kwenye Uhusiano na mpenzi wako unatakiwa kujiuliza maswali yafuatayo ili kuwa na uhakika na mahusiano kwamba upo katika mahusiano sahihi au unapoteza muda tu

Kumbuka maswali hayajajibiwa bali majibu unatakiwa kuyatoa mwenyewe kisha kuyafanyia kazi.

1. Unaufurahia uhusiano wako?
Hili ni swali la msingi kujiuliza. Ni vizuri ukajua kama unayo furaha katika uhusiano wako. Ukibaini kwamba hauko na furaha ujue kuna tatizo na uamuzi utakuwa si kuendelea kumng’ang’ania huyo uliyenaye bali unatakiwa kumuacha.

Kumbuka maisha yaliyotaliwa na huzuni hayawezi kuwa marefu, unaweza kujikuta unafupisha maisha yako kwasababu ya mapenzi tu. Kwa maana hiyo leo hii kaa na ujiulize kama unaufurahia uhusiano wako ama laa, isiwe bora liende tu.

2. Uko tayari kwa mtoto?
Hili si kwa walioolewa/walioa tu bali hata walio katika uhusiano wa kawaida.

Uko na mpenzi wako, kaa jiulize kama unadhani ni wakati muafaka kujiachia kwake ili upate mtoto kabla ya kuoana? Ukiwa makini suala la kupata mtoto haliwezi kutokea kama ajali ni ishu ya kuamua tu.

Kama uko ndani ya ndoa pia, ni kweli mtoto ni sehemu ya furaha katika maisha yenu lakini unadhani mmejipanga kwa kulea kwa muda huu? Usifanye mambo kibubusa, jiulize kisha jibu utakalolipata ulifanyie kazi.

3. Lipi la kujibadilisha?
Chukulia kwamba umepewa nguvu ya kujibadilisha vile ulivyo. Unadhani ni kitu gani ambacho unahisi kinamkwaza mpenzi wako au kinamboa lakini huwezi kukiacha?

Naamini kipo hivyo kama utakibaini ni vyema ukakifanyia kazi hata kabla hujapewa nguvu hiyo ya kujibadilisha kwani kuendelea kuwa hivyo ni kuliathiri penzi lako.

4. Kipi kinakufanya uhisi unapendwa?
Unahisi huyo uliyenaye anakupenda? Kama ndiyo ni lazima ukae na kujiuliza sababu za kukufanya uhisi hivyo.

Unadhani ni kutokana na mambo unayomfanyia, muonekano wako au tabia zako? Haiwezekani ikawa unahisi tu kwamba huyo uliyenaye anakupenda bila sababu za msingi.

Ukishabaini yale yanayokufanya uamini kwamba anakupenda basi tia chumvi, hakikisha hutoki kwenye mstari, mtadumu.

5. Kipi kinakuchukiza sana kwa mpenzi wako
Huenda vipo vitu vingi vinavyokuchukiza kwa mpenzi wako, hilo siyo tatizo kubwa kwani huo ndiyo udhaifu tunaousema kwamba kila mmoja anao.

Huwezi kumpata mpenzi ambaye atakufurahisha kwa kila kitu, ni lazima yatakuwepo mambo kadhaa ambayo huyafanya na huwa yanakuchukiza. Katika hayo angalia moja kubwa kuliko yote kisha uanze nalo katika kukabiliana nayo.

Naamini si ya kukufanya uachane naye ila ukiyajua itakuwa ni rahisi kuyazoea kwani inawezekana naye ni vigumu kuyaacha mara moja.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot