NMB yazindua mpango wa AgriBiashara, yatenga Bilioni 500 kusaidia wakulima nchi nzima - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, August 6, 2016

NMB yazindua mpango wa AgriBiashara, yatenga Bilioni 500 kusaidia wakulima nchi nzima

Mkurugenzi Mkuu wa NMB, Ineke Bussemaker(Wa kwanza kulia) akishikilia bango la Agri Biashara kuashiria kuzinduliwa kwa Programu hiyo iliyotengewa zaidi ya sh.Bilioni 500. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa AgriBiashara, Renatus Mushi na Katikati ni Mkurugenzi wa Kitengo cha AgriBiashara, Seif Ahmed.

Na Mwandishi Wetu
BENKI ya NMB imezindua Program Maalum yenye lengo la kuinua na Kuendeleza Sekta ya kilimo ijulikanayo kwa jina la Agribiashara inaogharamu kiasi cha Bil.500
Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam jana Mkurugezi Mkuu wa Benki hiyo, Ineke Bussemaker alisema benki hiyo inatambua kuwa zaid ya asilimia 60 ya watanzania wamejiajiri katika kilimo hivyo imewapelekea wao kuweza kutenga kiasi hicho cha fedha ili kuweza kufanya kilimo kuwa endelevu hapa nchini. 
"Upatikanaji wa huduma za fedha za kuweza kuwasaidia hawa watu waliojikita katika tasnia ya kilimo umekuwa ni wa shida hivyo basi tumeamua kutenga kiasi hicho cha fedha ili kuweza kuwasaidia wale wote wenye uwezo wa kufanya kilimo hivyo mpango huu tuliozindua utapelekea njia mbadala ya bunifu katika upatikani wa mtaji katika kukuza sekta hii ya kilimo’’,alisema.
Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker akizungumza kuhusu mpango wa AgriBiashara ambao utawanufaisha wakulima nchini kutokana na utolewaji wa kiasi kikubwa cha fedha kwa watu hao.

Bussemaker alisema kwa kuzingatia umuhimu wa kuboresha sekta ya kilimo Tanzania wameamua kujenga mazingira ambayo mkulima mdogo na washiriki wake wataweza kuboresha ufanisi katika upatikanaji wa pembejeo,uzalishaji kwa njia ya kisasa na ufanisi kwenye masoko kwa uhakika wa upatikanaji wa fedha za kilimo.
Aliongeza kuwa hapo awali benki hiyo ilikuwa ikitoa fedha kwa mazao makuu manne pekee lakini kwa hivi sasa wamepanua wigo kwa kuweza kutoa fedha kwa wakulima wanaolima mazao zaidi ya 12 na kuongeza kuwa hata wale wauzaji wa pembejeo na wengineo wataweza kupatiwa fedha hizo ili ziweze kusaidia sekta hiyo ya kilimo ambayo imeonekana kuwa ndio kitovu cha ukuaji wa uchumi hapa nchini.
 Pia Bussemaker alisema kuwa Benki hiyo haina lengo la Kushindana na Benki zilizokuwa mahususi katika masuala ya kilimo hivyo wao watashirikiana vyema na benki hizo pamoja na Serikali ili kuweza kufanikisha malengo waliyojiwekea Serikali.
 Hata hivyo Mkuu wa kitengo cha Kilimo biashara Renatusi Mushi alisema sekta hii ina msukumo chanya kwenye maisha ya wakulima hivyo tayari NMB imewafikia wakulima wadogo wasiopungua 600,000 nchi nzima kwa lengo la kuonyesha umuhimu wa sekta hii katika kukuza kipato ndani na nje ya nchi kwa kujaji wakulima na wafanya biashara .
 Mushi alisema NMB pia hutoa elimu ya fedha na mfunzo ya biashara kwa Watanzania ikiwemo na wakulima wakubwa,wafanya biashara wa Pembejeo na wachakataji wa mazao ya kilimo ili kuwajengea uwezo wa namna bora ya kusimamia mapato yao.
Mkuu wa AgriBiashara, Renatus Mushi akizungumza jambo na waandishi wa habari hawapo pichani juu ya program hiyo waliyoianzisha

 "Kilimo ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania kutokana na kuchangia 70% wa kipato cha kaya na vijijini,huajiri 75% ya Watanzania na kuchangia wastani wa 26% ya pato la taifa, sekta hii inakuwa kwa watani wa 4% kwa mwaka jambo hili linaloonyesha matumaini japo kuna mengi ya kuboresha katika sekta hii,"alisema.
 Aliongeza kuwa Fedha zilizotengwa na Benki hiyo zitakuwa zikitolewa katika matawi ya benki hiyo kwa wateja wa benki hiyo na hata wale wasio wateja

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot