![]() |
| Rais wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Jamali malinzi |
Na Carlos Nichombe
Rais wa Shirikisho la soka nchini (TFF) Jamali malinzi ameziomba klabu zinazoshiriki Ligi Kuu pamoja na Ligi Daraja ya Kwanza kutumia fursa ya michuano ya Airtel Rising Stars kwa ajili ya kujipatia wachezaj walio na uweledi mkubwa wa maswala ya soka.
Aliyasema hayo Dar es Salaam jana alopokuwa akifungua Mashindano hayo ya kusaka vipaji vya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Airtel Rising Stars kwa ngazi ya mkoa ambayo yameanza kutimua vumbi hapo jana.
Alisema kuwa michezo hiyo imekuwa ikitoa nafasi kwa vijana mbali mbali waliochini ya miaka 17 kuonyesha vipaji vyao hivyo kuzitaka klabu zote nchini kutumia vyema fursa hiyo ili kuweza kuepukana na matatizo ya migogoro ya wachezaji inayotokea hivi sasa.
" Michuano hii inatoa nafasi nzuri kwa klabu zetu kuja na kutambua vipaji vinavyoibukia na kuwasajili kwenye timu zao ili waweze kupata vijana wenye ubora na kuepusha matatizo yanayotokea mara kwa mara ya kunyang'anyana wachezaji, pia niwaombe vijana wetu wajitume kwa bidii ili kuweza kutimiza ndoto zao za kuwa wachezaji nyota nchini na Duniani kwa ujumla," alisema Malinzi.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo, Mkurungenzi Mtendaji wa Airtel Tanzania, Sunil Colaso aliwashukuru wadau wa soka kwa kusaidia na kushiriki kwao kwenye michuano ya Airtel Rising Stars kwa miaka mitano na kuwaomba makocha kuwachangua wachezaji wenye vipaji kwa ajili ya kuandaa timu ya kushiriki michuano ya taifa.
Aliongeza kuwa viongozi wa soka kutoka Mikoa yaKisoka ya Ilala, Temeke na Kinondoni kutumia vyema
fursa hiyo na kuacha kuongopa miaka ya vijana wanaoshiriki katika michuano hiyo ili kuweza kuinua soka la hapa nchini.
‘Tunajivunia uhusiano wetu mzuri na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na Afrika kwa ujumla
na tunayo furaha kuwa Klabu na Timu za Taifa zinafaidika na matunda ya Airtel Rising Stars’ lakini niwaombe viongozi wa soka kutoka kwenye mikoa yetu inayoshiriki kuwa wawazi na kushirikiana vyema na Kampuni pamoja na Shirikisho ili kuweza kuinua sekta hii ya michezo," alisema Colaso
Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi mapema leo hii kwa kwa kuzikutanisha timu za Ilala Boys pamoja na
Bom Bom Boys ambazo ziliweza kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na kuzifanya timu hizo zitoke
uwanjani kwa kugawana pointi moja moja.
Bao la Timu ya Ilala Boys lilifungwa na Hamza Nazali dakika ya 45 na timu ya Bom Bom bao lake lilipatikana kupitia kwa mchezaji wake Kiema Juma mnamo dakika ya 55.
Waamuzi waliochezesha michuano hiyo ni Hashim Omary(Mwamuzi wa Kati), Abdallah Said(Mwamuzi wa
kushoto), Yahaya Hamid(Mwamuzi wa kulia), Said Mtitu(Mwamuzi wa akiba) pamoja na kamisaa, Juma
Athumani.
Michuano ya Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa ikishirikisha Ilala, Temeke, Kinondoni, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Lindi, Zanzibar na Arusha itafikia tamati wakati wa fainali za taifa zitakapofanyika kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam tarehe 6 mpaka 11 Septemba mwaka huu.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF Salum Madadi waliwapongeza Airtel kwa program hii huku akisema imesaidia kutafuta na kukuza vipaji vya soka nchini.



No comments:
Post a Comment