Zitokabwe afunguka ya moyoni kuhusu CCM - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, July 24, 2016

Zitokabwe afunguka ya moyoni kuhusu CCM


Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe.
Na Mwandishi Wetu.

Zito kabwe amefunguka mambo mbali mbali yakihusucho chama cha Mapinduzi mara baada ya kukamilika kwa mchakato wa kumpata Mwenyekiti wao mpya wa chama hicho ambacho ndio kinaiongoza Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Zito kabwe aliyasema hayo kupitia akaunti yake ya Facebook ambapo ametoa tahadhari kwa vyama vya upinzani kuwa macho na CCM inayoongozwa na Mwenyekiti wao Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ndio rais wa nchi hii.

"Unashangaa ya Mrema ( TLP ) na Cheyo ( UDP )? Kama ni msomaji wa Siasa za Dunia wala hutasumbuka maana Ni mambo yamefanyika sana. Hao ndio systemic opposition.

Jambo la muhimu ni kujua kuwa Rais wa sasa sio yule aliyemtangulia na hivyo CCM ya kuanzia Leo haitakuwa CCM iliyoishia Jana. Rais anayeweza kutamka hadharani kuwa ' angewapoteza' watu, tena wanachama wa Chama chake, kwa kuonyesha kutokukubaliana na Maamuzi ya chama ndani ya vikao vya Chama, ni mtu hatari na hivyo mbinu za kushindana naye lazima ziwe tofauti. 

Huu ndio wakati wa kujenga Mfumo madhubuti wa Vyama vingi kuliko wakati mwengine wowote katika historia ya Nchi yetu. Nasaha zangu kwa Viongozi wote wa upinzani ni ' tujisomee kwanza '! Tujue mbinu na medani. Pia Sisi tuwe ' more democratic ' kuliko CCM kwa kuruhusu maoni tofauti kwenye Vyama vyetu badala ya kuwa na tabia zile zile za CCM. 


Mrema na Cheyo wamekuwa wenyeviti wa Vyama vyao tangu Mwinyi ni Mwenyekiti wa CCM na bado hawaoni haya wala soni kusifia CCM na mfumo wao wa kubadilishana Uongozi. Cheyo alikuwapo Mwinyi alipomkabidhi Mkapa, Mkapa alipomkabidhi Kikwete na Kikwete alipomkabidhi Magufuli! Kote huko alitoa hotuba. Wachambuzi wa Siasa wangechambua hotuba za Cheyo miaka yote hiyo na kumwuliza anajisikiaje! 


Uenyekiti wa Magufuli CCM ni faida kwa mfumo wa Vyama vingi kwani Upinzani wa kweli utaimarika. Upinzani wa Hoja na Masuala utaimarika zaidi kuliko wakati mwengine wowote.


Huu ndio wakati wa kusambaza Azimio la Tabora linalohuisha Azimio la Arusha".

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot