Na Mwandishi wetu.
Baada ya Rais Magufuli kutangazwa kuwa ameshinda na kuwa ndiye
Mwenyekiti wa tano wa CCM Taifa akichukua nafasi iliyokuwa inashikiliwa
na Rais wa awamu ya nne, Dkt Jakaya Kikwete, Mbunge wa Kigoma Mjini na
Kiongozi Mkuu wa ACT- Wazalendo ameandika haya kwenye ukurasa wake wa
Facebook;-
“Napenda kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuchaguliwa kwake
kuwa Kiongozi wa Chama chake cha CCM akiwa Mwenyekiti wa Tano chama
hicho. CCM imeendelea kudumisha utamaduni wa kukabidhiana Uongozi kila
baada ya muda.
Jambo ambalo ni la kujifunza hasa kwa vyama vya Siasa nchini na
barani Afrika. Nataraji kwamba Rais na Mwenyekiti mpya wa CCM ataona
umuhimu wa Vyama vya Siasa kuendelea kufanya Siasa bila vikwazo na kwa
mujibu wa Sheria za Nchi yetu.
Demokrasia inaimarisha Amani kwa kupaza sauti za HAKI. Karibu kwenye changamoto za kuongoza Vyama vya Siasa ndugu Rais.”
Pia alisema hivi
"Zanzibar
sasa iwe ajenda ya kudumu kwa Vyama vyote vya Siasa vinavyosimamia
HAKI. Rais Magufuli hawezi kukwepa tena suala la Zanzibar kwani sasa ni
Mwenyekiti wa Chama chake. Hana excuse tena. Suala la Zanzibar sio la
CUF peke yao, ni suala letu sote. Shime wana demokrasia"
|
|



No comments:
Post a Comment