KAMPUNI ya Tanzania Breweries Limited (TBL) imezindua bia mpya inayojulikana kama Ndovu Red Malt, ambayo imetengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100 na ikiwa ni mwendelezo wa ubunifu wenye ubora wa bia ya Ndovu Special Malt inayoongoza kwa ubora na bia pendwa kwa watumiaji wengi wa bia nchini.
Akizungumza katika uzinduzi huo Dar es Salaam jana ,Meneja Masoko wa vinywaji wa kampuni ya TBL Vimal Vaghmaria alisema kuwa Bia hiyo imegundulika na kutengenezwa hapa nchini ili kukidhi ladha ya wanywaji ikiwa na ubora wa kiwango cha juu na yenye ladha ya pekee kwa kulinganisha na aina nyinginezo za bia zilizopo kwenye soko.
![]() |
| Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Damian Soul akitoa burudani katika uzinduzi wa bia ya Ndovu Red Malt, Picha na Prona Mumwi |
Uzinduzi huo ulifanyika katika mgahawa wa 305 The Boks uliopo Kinondoni jijini hapa ambapo wateja zaidi ya 50 walihudhuria katika hafla ya uzinduzi wake.
“Ubunifu wa kila bidhaa yetu unalenga kukidhi matakwa ya watumiaji wake ambao ni wateja wetu ambao wanahitaji kutumia bia zilizo bora na zinazokwenda na wakati katika soko,Mbali hiyo ladha ya aina yake inayoleta burudani kwa watumiaji wake kutokana na kutengenezwa kwa Shahiri kwa asilimia kubwa pia bia ya Ndovu Red Malt inavutia kwa mwonekano wake wa rangi kuwa na rangi ya uwekundu kwa mbali"alisema .Vaghmaria
Kwa upande wake, Mpishi Mkuu wa Bia hiyo TBL, Cavin Nkya, alisema kuwa bia hii mpya ya Ndovu Red Malt inazinduliwa ikiwa ni uthibitisho wa uwezo wa kampuni katika kuwapatia watanzania kinywaji chenye kiwango cha kimataifa na chenye ubora wa hali ya juu.
“Ndovu Red Malt ni bia ya daraja la kwanza inayodhihirisha dhamira yetu ya kuwapatia wateja kinywaji ambacho daima wametamani kukipata kikiwa kimesheheni radha murua na ya kipekee,” alisema Nkya.
Aliongeza kuwa matokeo mazuri katika utayarishaji wa kinywaji hicho ni kutokana na uchanganyaji mahiri na wa umakini wa nafaka bora zinazozalishwaa hapa nchini ambazo zinazotumika kutengeneza bia hiyo.
"Bia hii ina kiasi cha kilevi cha asilimia asilimia 4 na inapatikana katika chupa zenye muundo maridhawa zenye ujazo wa mililita 375 ,kama zilivyo aina nyingi za bia zinazozalishwa na kampuni ya TBL zilizopo sokoni hivyo itaanza kupatikana kwa kuanzia wiki hii na kwa Gharama ya Tsh,2000 kwa rejareja"alisema




No comments:
Post a Comment