KATIKA kusogeza huduma zake karibu,Benki ya Amana imezindua Kitengo cha huduma kwa wateja kitakacho mwezesha mteja kupata huduma na taarifa zinazo husiana na benki hiyo.
Akizungumza Dar es Salaam jana,Meneja Mfawidhi huduma kwa wateja katika Benki hiyo Juma Msabaha alisema kuwa lengo ni kusogeza huduma kwa wateja,kupokea maoni mbalimbali kuhusiana na huduma pamoja na maboresho zaidi.
Alisema kituo hicho kitasaidia kuboresha taarifa za huduma za moja kwa moja ikiwemo ATM,huduma za kibenki kwa njia ya Simu,pamoja na miamala ya kifedha ambazo zinatumiwa na wateja.
"Lengo la huduma hii itaongeza mahusuasiano mazuri baina ya mteja na benki ,hivyo wateja watumie kituo hicho kama njia sahihi ya kufikisha malalamiko,maoni na maboresho kwa benki yetu"alisema Msabaha.
Kwa Upande Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo Munir Rajab alisema kwa sasa wanampango wa kuongeza matawi katika maeneo mbalimbali ya nchi ili kuongeza wigo mpana wa kuwahudumia wateja.
Alisema wanampango wa kufungua matawi mawili ikiwemo Zanzibar ambapo benki hiyo haikuwepo kwa upande wa visiwani na bara itafunguliwa moja katika mkoa wa Tanga.
"Kwa sasa benki yetu inamatawi saba ambapo matano yapo katika mkoa wa Dar es Salaam ,Mwanza moja na Arusha hivyo wateja wetu waendelee kutumia huduma zetu kwani tunatoa huduma zenye ubora tofauti na benki nyingine"alisema Rajab



No comments:
Post a Comment