Azam FC Yamnyakua Nyota Medeama - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Saturday, July 30, 2016

Azam FC Yamnyakua Nyota Medeama

Enock Atta Agyei
Enock Atta Agyei

Na Carlos Nichombe.

KLABU ya Azam FC imefanikiwa kunasa saini ya winga wa Medeama ya Ghana, Enock Atta Agyei, na kusaini mkataba wa miaka miwili.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa Azam, kinda huyo alilivutia benchi la ufundi la Azam wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga uliochezwa Uwanja wa Taifa na kupendekeza asajiliwe.
Uongozi wa Azam FC umefanya jitihada na kunasa saini yake chini ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Saad Kawemba, aliyeenda Ghana kukamilisha kazi hiyo kwa kuzungumza na pande zote mbili mchezaji na uongozi wa Medeama akiwemo mmiliki wa timu, Moses Armah.
Pia Kawemba alipata fursa ya kukutana na Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Ghana ‘Black Stars’, Avram Grant raia wa Israel, na aliipongeza Azam kwa kutambua kipaji cha Enock na kumsajili.
“Nawapongeza Azam kwa kutambua kipaji cha Enock, nawaahidi nitakuwa namfuatilia kwa karibu kwa kipindi chote cha mkataba wake atakachokuwa Azam FC,” alisema Grant katika moja ya mazungumzo yake na Kawemba.
Enock, mwenye miaka 18 na kipaji cha kusakata kabumbu mara baada ya kukamilisha taratibu zote anatarajia kutua nchini leo asubuhi na ndege ya Shirika la Kenya (KQ).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot