![]() |
| KAMISHNA Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Makao Makuu ya kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania (SACP) Fortunatus Musilimu akitoa ufafanuzi kwa madereva boda boda hawapo pichani. Picha Na Carlos |
Na Carlos Nichombe
KAMISHNA Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Makao Makuu ya kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania (SACP) Fortunatus Musilimu amewataka waendesha bodaboda kufuata taratibu na sheria za usalama barabarani ili kuweza kupunguza tatizo la ongezeko la ajali nchini.
Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana baada ya kukamilisha ziara ya kuwatembelea wagonjwa waliopata ajali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyoandaliwa na Vyama vya Bodaboda wilaya ya Ilala,Temeke pamoja na Kinondoni.
Alisema waendesha bodaboda wamekuwa wakipata ajali za mara kwa mara, na ajari hizo zimekuwa zikisababishwa na madereva wenyewe kwa kuendesha vyombo hivyo pasipokufuata taratibu na sheria za usalama barabarani ikiwemo kuendesha vyombo hivyo wakiwawamelewa.
“Zipo sheria na taratibu zinazo waongoza hawa watu wa bodaboda lakini wengi wao wamekuwa hawazifuati kabisa, kwamfano kwenye mataa yaliyopo sehemu mbali mbali za barabara hatakama alama inawaashiria kusimama wao watataka kupita tu na mwisho wa siku wanapata ajali, lakini endapo watazifuata taratibu zote walizofundishwa wakiwa chuo kutapelekea kupungua kwa hili tatizo la ajali za mara kwa mara zinazowakuta na pia kutairejeshea heshima sekta hii ya usafirishaji ya bodaboda,” alisema Musilimu.
Pia aliwataka madereva wanaoendesha vyombo vya moto pasipo kupata mafunzo kuacha mara moja
kwani kitendo hicho ni kinyume na sheria na endapo watabainika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo kifungo au kulipa faini pamoja na kushikilia vyombo vyao.
Akizungumza kwaniaba ya Madereva bodaboda Afisa Habari wa Bodaboda wilaya ya Ilala, Abdallah Bakari alilalamikia kitendo cha ulinzi shirikishi kuwakamata kwa kutumia nguvu pindi wawapo barabarani nakusababisha ajali zinazo hatarisha uhai wa madereva hao.
Alisema kuwa Bodaboda zimetoa fursa ya ajira kwa vijana waliokosa ajila na kulitaka jeshi la polisi kwa ushirikiano na TAMISEMI kutengeneza mazingira yatakayowafanya madereva hao kufanya kazi zao kwa uhuru.
Kwa upande wake Daktari bingwa wa Magonjwa ya ajali na Mifupa MOI, Kennedy Nchimbi aliwataka madereva bodaboda kujiunga na mifuko ya bima ya afya ili iweze kuwasaidia kupata matibabu kwagharama nafuu pindiwapatapo ajali na katika maisha yao yakawaida.
Alisema kumekuwa na idadi kubwa ya madereva wa bodaboda wanaoshindwa kumudu gharama za matibabu kutokana na vipato vyao kuwa duni hivyo kama wataweza kujiungana mifuko yabima ya afya pamoja na hifadhi za kijamii zitawasaidia kupata huduma ya matibabu pamoja na pensheni mbalimbali zitolewazo na mifuko hiyo zitakazo wawezesha kuendesha maisha yao.



No comments:
Post a Comment