WANARIADHA wa Timu Teule ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ imemuahidi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kurejesha heshima katika Michezo kwa kuleta medali nyingi kutoka Rwanda.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na Wanariadha hao walipotembelewa na Mkurugenzi wa Michezo na Utimamu wa Mwili wa JWTZ Brigedia Jenerali Martin Busungu katika kambi yiliyowekwa Katika eneo la Sanu Baray Wilayani Mbulu Mkoani Manyara.
Walisema Maandalizi ya Safari hii kuelekea mashindano ya Afrika Mashariki yanayotarajia kufanyika Agosti Mwaka huu Nchini Rwanda ni Maandalizi ya kina ukizingatia Jeshi likiwa limewawezesha ipasavyo hivyo hawana sababu ya kukosa ushindi.
Jackline Sakilo ambaye ni mmoja wa wanariadha tishio alisema kambi imewekwa katika eneo ambalo lina hali ya hewa inayoruhusu, ambayo ni Futi 1980 kutoka usawa wa bahari hivyo Mkuu wa majeshi ajiande kupokea medali kutoka kwa Vijana wake .
Aliongeza kuwa Jeshi linamategemeo kwa Wachezaji wote wa Timu teule za Jeshi lakini pia Wananchi kwa ujumla wanategemea Timu yao itafanya vyema hivyo wanapaswa kupigana vilivyo kuibuka na ushindi kwa kila Mchezo.
Brigedia Jenerali Busungu aliongeza kuwa amesikia ahadi ya wachezaji ya kupata ushindi na kuleta medali nyingi na kuwapongeza kwa ahadi hiyo na kutaka sasa ikafanyike kwa vitendo.
Mashindano ya Majeshi kwa Nchi za Afrika Mashariki yanatarajiwa kufanyika Kigali Nchini Rwanda kuanzia Agosti Saba hadi Agosti 17 Mwaka huu Nchini Rwanda huku Tanzania katika Riadha itapeleka Wanariadha 12 Wanawake Sita na Wanaume Sita.


No comments:
Post a Comment