Azam kambini Zanzibar leo - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, July 24, 2016

Azam kambini Zanzibar leo

Kikosi kazi cha Timu ya Azam F.C kikiwa katika Picha ya Pamoja baada ya kumalizika kwa mazoezi yaliyofanyika uwanja wa timu hiyo.

Na Mwandishi Wetu

AZAM FC inaondoka leo kuelekea visiwani Zanzibari kwajili ya kuweka kambi kwa maandlaizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya vodacom unaotarajiwa kuanza badaye Agosti mwaka huu.

Msemaji wa timu hiyo Jaffar Maganga alithibitisha uwepoo wa safari hiyo kuelekea visiwani humo na kwamba kambi hiyo ni maombi maalumu ya kocha wao ambaye aliomba kwa viongozi kupata kambi ya nje ya mji katika kuwajenga wachezaji kisaikolojia.

Azam inakwenda huko baada ya kucheza michezo kadhaa ya kirafiki katika kujipima nguvu na kushinda yote ambapo walianza kwa kuifunga Ashanti baadaye wakaibugiza Friends Rangers na mwishoni mwa wiki kuifanyia maangamizi timu ya Kinondoni.

Azam ilifunga timu ya Halmashauri ya Kinondoni (KMC) mabao 5-0 Uwanja wa Azam Complex, Azam Dar e s Salaam mwishoni mwa wiki.

Shukrani kwao, wafungaji wa mabao hayo, Nahodha John Raphael Bocco, kiungo Mudathir Yahya Abbas mawili, Shaaban Iddi na Farid Mussa.

Bocco alianza kufunga dakika ya tatu akimalizia kwa shuti kali pasi ya Shaaban Idd, kabla ya Mudathir Yahya kufunga la pili dakika ya sita akimalizia pasi ya Fuadi Ndayisenga aliye kwenye majaribio Azam FC.

Mudathir akawainua tena vitini mashabiki wa Azam kufung bao la tatu dakika ya 14 kwa shuti kali akimalizia pasi ya Salum Abubakar ‘Sure Boy’ na Shaaban Idd akaipatia bao la nne Azam FC akitumia vema pasi ya Bocco.






Wachezaji wa Timu ya Azam wakiwa katika moja kati ya mazoezi ya timu hiyo, picha kwa hisani ya Azam F.C

Zikiwa zimesalia dakika mbili mchezo kumalizika, Mudathir Yanga akawafungia tena Mabingwa hao wa Afrika Mashariki na Kati bao la tano.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot