![]() |
| Ni moja kati ya maeneo yaliyoathirika kutokana na mvua pamoja na kimbunga huko nchini China. |
Na Carlos Nichombe
Vyombo vya habari nchini China
vinasema kuwa zaidi ya watu 50 wameauwa kufuatia kutokea kimbunga na
mvua kubwa katika mkoa ulio mashariki mwa nchi wa Jiangsu.
Sehemu nyingi za nchi zimekumbwa na mvua kubwa wiki hii. Mafuriko kati kati mwa China yamesababisha karibu watu 200,000 kuhama makwao.
Mamlaka ya Hali ya hewa ya nchi hiyo imetahadharisha wananchi kuwa makini kwa sasa kutokana na hali ya hewa kutokuwa nzuri.



No comments:
Post a Comment