Waziri wa Utalii Brazil ang'oka - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 16, 2016

Waziri wa Utalii Brazil ang'oka

Waziri wa utalii nchini Brazil,Henrique Alves aliye jiuzuru hivi karibuni kutokana na shutuma zinazomkabili.

Waziri wa utalii nchini Brazil,Henrique Alves amejiuzulu siku moja baada ya kushutumiwa kujihusisha katika kampeni zisizo halali za kujipatia fedha kutoka kwa wanyonyaji wakubwa wa rushwa wa taifa wa kampuni ya mafuta, Petrobras. 

Alves ni waziri wa tatu kujiuzulu katika wa utawala wa raisi Michel Temer ambaye yuko katika muhula wa serikali iliyojaa kashfa.

Waziri Alves akiwa bado anazipinga tuhuma hizo bado Taasisi mbalimbali zimeweza kuendelea kutoa ushahidi wao mahakamani ili kuweza kuwabaini na kuwachukulia hatua wale wote waliohusika katika kufanya vitendo vya rushwa nchini humo.

Jumatano ,mahakama kuu imetoa ushaidi kutoka kwa mmoja wa wakuu wa Pretrobas, Sergio Machado ambaye amewahusisha wanasiasa ishirini wenye majina makubwa akiwemo raisi Temer ambaye pia amepinga kuhusika kuwasaidia wanachama wa chama chake katika harakati hizo zisizo halali.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot