![]() |
| Wanafunzi wa Manispaa ya
Morogoro wakimba wimbo maalum wa siku ya mtoto wa Afrika huku wakiwaonyeshea wenzao ambao wanaigiza kama
walemavu kulia wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya mtoto wa
afrika. Picha na jumamtanda.blogspot.com |
Na Sekela Mwambene
TUME ya Haki za Binadamu na Utawala bora (THBUB) imelaani vikali vitendo vya kikatiri vinavyofanyika kwa baadhi ya watoto nchini, hivyo imeitaka jamii kuhakikisha kuwa inatoa kipaumbele kwa watoto wote nchini katika malezi ili kuwafanya wawe na malezi bora.
Pia imesema kuwa inasikitishwa na kukerwa na matukio ya aina mbalimbali wanayofanyiwa watoto ambayo yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara ikiwemo kutupa watoto wachanga,Ubakaji,Ulawiti,Mauwaji Ukeketaji,na Watoto wa kike kuozwa katika umri mdogo na kusababisha kukosa haki zao za msingi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Kamishna wa Tume hiyo Salma Hassan alisema kuwa kitendo cha kumuozesha mtoto chini ya umri mdogo ni kumkosesha haki za msingi hususani haki ya kupata elimu ambapo vitendo hivyo vinafanywa na watu wenye akili timamu.
"Tunapo adhimisha siku ya mtoto wa afrika tukumbuke kuwalinda watoto kwa tukiwalinda tutaweza kuwafanya waweze kukuwa katika maadili mazuri na hususani katika kupata haki za msingi ikiwemo elimu kwa matendo ya ukatili hufanywa na watu wenye akili timamu hivyo tuwalinde kwa nguvu" alisema.
Alisema kumbukumbu ya siku ya mtoto wa Afrika hufanyika kila mwaka ikiwa ni mara ya 26 tangu umoja wa Nchi huru za Afrika OAU izindue siku hiyo mwaka 1991 ambapo nchi yetu ilisaini na kulidhia mikataba ya kimataifa ma kutunga Sheria mbalimbali za kuharalisha makosa ya ukatili dhidi ya Binadamu.
"Tume inasisitiza kuwa binadamu wote huzaliwa huru,na wote ni sawa ambapo kila mtu anastahili heshima na kutambua utu wake amapo itaambuliwa katika ibara ya 12 ya katika ya jamuhuri ya muungano wa tanzania ya mwaka 1977"alisema Salma .
Aliongeza kuwa Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa haki za watoto kuunganisha nguvu kupinga vitendo vya kikatili dhidi ya watoto vinavyo fanyika mahali popote Tanzania.



No comments:
Post a Comment