watu nane wauwawa Uganda - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 16, 2016

watu nane wauwawa Uganda

Gari ya Jeshi la polisi uganda,picha na mtandao

Jeshi la Nchi ya Uganda imeripoti watu nane kuuwawa na Askari katika tukio linalosemekana ni la kutumia hasira.

Msemaji wa jeshi la Uganda meja Edward Birungi, anasema kuwa mwanajeshi huyo anaripotiwa kutofautiana na mkewe.

Anaripotiwa kuwa mlevi na alikuwa pia amevuta bangi akiwa kazini, ambapo alianza kufyatua risasi kiholela akimtafuta mkewe ambaye alifanikiwa kutoroka.

Wanawake wanne akiwemo mwanajeshi waliuawa wakati wa kisa hicho.

Wengiwe waliouawa ni pamoja na wake wa wanajeshi wengine, wakiwemo pia watoto watatu.

Mwanajeshi huyo naye aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wengine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot