Na Sekela Mwambene
TANZANIA inatarajia kuwa Mwenyeji wa Maadhimisho ya 6 ya wiki ya Maji Barani Afrika ambayo yataambatana na maonyesho ya Wadau wa Sekta mbalimbali za Maji na Umwagiliaji.
Pia inatarajia kuwa mwenyeji katika mkutano wa 10 wa Baraza la Mawaziri wa maji wa nchi za Afrika ambapo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani anatarajia kufungua mkutano huo.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana,Mkurugenzi msaidizi wa Maji shirikishi kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Sylvester Matemu alisema kuwa mkutano huo unatarajiwa kufanyika Julai 18 hadi 22 mwaka huu katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Alisema mkutano huo utahudhuriwa na washiriki zaidi ya 1000 kutoka nchi 54 za bara la afrika na dunia kwa ujumla ambapo Waziri mkuu Majaliwa Kassimu Majaliwa anatajia kufungua maonyesho hayo.
Alisema katika maadhimisho hayo wataweza kushuhudia teknolojia mbalimbali,kubadirishana uzoefu na wataalamu kutoka nchi mbalimbali ili kuweza kuunga mkono juhudi za maendeleo ya Sekta ya maji na umwagiliaji.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni "Kufikia Lengo la Maendeleo endelevu Juu ya Usalama wa Maji na Usafi wa Mazingira"
Mwisho.


No comments:
Post a Comment