![]() |
| Naibu Spika wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania |
Na Rachel Balama
UMOJA wa Wanawake Viongozi wa Vyama vya Upinzani visivyo na Wawakilishi Bungeni wamepinga shinikizo lililotolewa na baadhi ya wabunge la kumtaka Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson kujiuzulu kwa kuwa sababu zilizotolewa hazina mantiki yoyote kwa taifa bali ni ukandamizaji dhidi ya wanawake.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana, Makamo Mwenyekiti wa Umoja huo, Cecilia Augustino,alisema kuwa Dkt. Tulia anafanya kazi kwa kufuata kanuni hivyo mashinikizo ya kumtaka ajiuzulu, kususia vikao, kutoa lugha za kuuzi, kejeli,dharau na kuzalilishana havina tija kwa taifa.
Alisema kuwa wao kama wanawake wameguswa na tabia ya mfumo dume kwa sababu zinazotajwa za kumshinikiza Dkt. Tulia atoke madarakani kwa kuwa sababu zilizotolewa hazina mantiki kwao na taifa kwa kuwa watanzania walitarajia kuona wabunge wao wakijenga hoja zenye maendeleo katika majimbo yao na kwa taifa na kwamnazenye maendeleo
Alisema kuwa kutokana na hali hiyo wanaona kuwa bado kuna changamoto nyingi zinazomkabili mwanamke na kwamba Dkt. Tulia anafanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni za bunge.
"Kanuni zinazotumika bungeni zimetungwa na wabunge hao hao, sisi kama wanawake tunasikitika kuona kwamba awaoni na hawatambui usimamizi mzuri wa bunge unaofanywa na Naibu huyo badala yake unatafsiriwa vibaya na kumtaka ajiuzulu jambo ambalo ni kinyume na maadili ya uongozi," alisema.
Alisema kwa sasa shughuli za bunge zimetawaliwa na vituko, kebehi na dharau za makusudi kwa Dkt. Tulia vinavyoashilia kumdharau wazi wazi spika huyo ambaye ni mwanamke bila sababu za msingi.
Aliongeza kuwa nchi zinazoendelea wanaongea mikakati ili wanawake waweze kuongoza katika nafasi mbalimbali za maamuzi na kwamba hata kama kuna kasoro katika utendaji kazi wake hukumu yake si kususia bunge , kushika mabango na kutaka ajiuzulu badala yake wanatakiwa kujenga hoja ndani ya bunge kwa kufuata kanuni zinazozongoza bunge hilo.
Aidha wanawake hao waliwaomba wabunge wote wanawake na wale ambao wamesusia vikao vya bunge warudi bungeni na kuungana na wabunge wenzao kwa kufanya kazi ya wananchi kwani kumtaka Dkt. Tulia ajiuzuli ni kudidimiza na kukandamiza juhudi zinazofanywa na wanawake katika uongozi.
Viongozi hao wanawake pia wameunga mkono juhudi zinazofanywa na wabunge wa upinzani kwa kuibua hoja na changamoto mbalimbali na kusaidia bunge kuwa zuri na la mfano kwani bila wapinzani hakutakuwa na bunge lenye tija.
"Tunawaunga mkono wabunge wa upinzani kwa kujenga hoja zenye mashiko kwa taifa na jamii kwa ujumla hivyo tuwawaomba warejee bungeni wakajenge hoja zenye mashiko zaidi, kitendo cha kususia bunge kinaweza kuzorotesha maendeleo ya taifa," alisema.



No comments:
Post a Comment