CUF TEMEKE:Taslim ni mzigo - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, June 20, 2016

CUF TEMEKE:Taslim ni mzigo


Makamu Mwenyekiti wa Chama cha CUF Twaha Taslima
CHAMA Cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Temeke kimesema Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Twaha Taslima ni mzigo katika Chama hicho na aache kumbeza aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama hicho Prof.Ibrahim Lipumba kwa kuwa tangu achukue nafasi hiyo hajawahi kuhojiwa na Polisi hata katika kituo kidogo.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana wakati wa tamko la Jumuia ya Wazee wa Chama hicho Wilaya ya Temeke,Katibu wa Chama hicho wilayani humo Kaisi Kaisi alisema yeye ni mlezi wa Jumuia zote katika Wilaya hiyo lakini hajawahi kumuona Taslima kufika wilayani humo hata kujitambulisha kwa wanachama.

Alisema anashangazwa na kauli aliyoitoa Taslima kuwa katika uongozi wake wa miezi tisa alifanikisha kupatikana kwa wabunge 10 wakati kazi hiyo ilifanywa na Prof.Lipumba

"Hawajawahi kuhojiwa Polisi tena hata kituo kidogo hajaitwa,hafanyi vikao ikiwemo kutembelea hata Wilaya ya Temeke kuangalia utekelezaji wa kazi za Chama,hajapigwa hata siku moja na Polisi sasa huyu ni mpinzani kweli au anashirikiana na Serikali na sisi tunamwambia aache kushangilia matunda ya wenzake kwani waliumizwa na wengine kushitakiwa lakini yeye hajawahi kuwepo zaidi ya kusimamia kazi zake za uwakili"alisema Kaisi

Kaisi alifafanua kuwa miezi tisa aliyokaa madarakani hajawahi kufanya hata ziara lakini Maalim Seif Sharif Hamad tangu uchaguzi umeisha ule wa kwanza na wa pili alishafanya ziara maeneo yote ya Zanzibar kabla ya kwenda Ulaya lakini Taslima yupo ofisini hivyo anaonesha wazi kuwa mapambano hayawezi.

"Tunataka Prof.Lipumba alirudi kwani Katiba inamruhusu kufanya hivyo na barua aliyoandika ya kujiuzulu haijajibiwa hadi sasa lakini pia alichaguliwa na Mkutano Mkuu ambao haujawahi kukaa kama Katiba inavyotaka na CUF iatarudi nyuma chini ya Uongozi wa Taslima."alisema Kaisi

Aidha aliongeza kuwa yeye anaunga mkono kauli ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad kuwa suala la Prof.Lipumba litaamuliwa na vikao lakini pia lilipaswa kuzungumziwa na Viongozi wa Tanzania Bara akiwemo Naibu Katibu Mkuu Magdalena Sakaya.

"Kwa masikitiko huku Taslima akiwa mwanasheria ameeleza tofauti na Katiba ivyoelezea Kiongozi akijiuzulu lakini cha kushangaza wanakuja akina Mazrui kutoka Zanzibar kumzungumzia Prof.Lipumba na hao ndio wanaomkataa ili asiwate wale walioshinda katika Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba mwaka 2015 nafasi za majimbo na kupewa vyeti vya ushindi na ZEC wasiende mahakamani kudai ushindi wao.

Akizungumza kwa niaba ya Jumuia ya Wazee wa Chama hicho Wilaya ya Temeke, Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Bakari Mtanga alisema Prof.Lipumba alivunjwa mkono na Polisi kwa ajili ya wananchi lakini pia alikamatwa na Polisi ikiwemo kufikishwa mahakamani na zaidi alitatua matatizo mbalimbali ya Chama lakini sio Taslima.

"Tunakitaka Chama kifuate taratibu kwani Prof.Lipumba alifuata utaratibu lakini haiwezekani jambo hilo likigawe Chama na sisi kama Wazee tunahoji yale maswali aliyoulizwa Prof.Lipumba na Kamati ya Uongozi lini Baraza Kuu lilikaa na kumuhoji Prof.Lipumba na hakutokea?"alihoji Mtanga

Alisema watu wanaomkataa Prof.Lipumba hawakitakii mema Chama hicho kwa kuwa hakitakuwa na nguvu tena kwa siku zijazo na kuomba suala hilo likishindikana basi walirudishe kwa wanachama waamue.

Akisoma tamko la Jumuia hiyo,Mjumbe wa Jumuia hiyo Ally Mbonde alisema kutokana na ushauri waliopewa na wanasheria walibaini kuwa hakuna utata wowote iwe wa kisheria au kikatiba kwa Kiongozi aliyejiuzulu katika Chama chao kurudi katika Uongozi

"Prof.Lipumba ni mtu muhimu katika Chama chetu na kama wazee hatuungi mkono Prof.Lipumba kuita vyombo vya habari kujibu masuala aliyoulizwa na hiyo busara ya Kamati ya Uongozi ndio inayokigawa Chama sasa sisi tunataka vikao halali vijadili na kuamua suala hilo na hatuwezi kuvumilia jambo lolote la kumvunjia heshima kiongozi huyo lifanikiwe"alisema Mbonde

Mbonde aliongeza kuwa maswali yote waliyomuuliza Prof.Lipumba basi wamuite katika vikao na wanaamini kuwa atawajibu na watamuelewa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot