Nisha Atoa makavu - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 21, 2016

Nisha Atoa makavu

Mkurugenzi wa Kampuni Nisha's Film Production,ambaye pia ni Balozi wa watoto wanaoshi katika mazingira Magumu,Salma Jabu (Nisha) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Dar es Salaam jana, wakati wa kutoa taarifa kuhusu kufuturisha watoto waishio katika mazingira hatarishi kushoto ni Meneja wa Nisha's Film Production Myovela Mfuaisa,na mtoto Said Abdalah na Lazak Rashidi.Picha na Prona Mumwi

Na Carlos Nichombe

MSANII wa filamu nchini na balozi wa watoto waishio katika mazingira hatarishi, Salma Jabu(Nisha) amewataka wanaotoa misaada kwa watoto waishio katika mazingira magumu, Yatima, Pamoja na wale waishio wenye ulemavu kuacha tabia ya kutoa misaada hiyo kwa msimu bali wafanye hivyo wakati wote wapatapo nafasi.

Aliyasema hayo Dar es salaam jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali waliyonayo watoto hao wa mitaani na kuongeza kuwa hali yao kwa sasa sio shwari.

Nisha alisema kuwa kumekuwa na mazoea ya watu kuweza kuwasaidia watoto kwa misimu misimu ikiwemo katika mwezi huu wa ramadhani kitu ambacho kinatoa faraja ya kipindi kifupi kwa watoto hao na pindi wamalizapo kipindi hicho wamekuwa wakiendelea na matatizo yaliyokuwa yakiwasumbua.

Alisema watoto wamekuwa wakihitaji msaada toka kwa watu wenye uwezo wakati wote ikiwamo ule wa kuwasaidia makazi, chakula, elimu pamoja na kushughulikia afya zao.


Hata hivyo Nisha ameandaa Futari kwa watoto waishio katika mazingira magumu,yatima na walemavu itakayotolewa siku ya jumapili kuanzia saa 10 jioni hadi 02 usiku itakayofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Azania na kuuzuliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu pamoja na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam.

"Siku hii tunawakaribisha watu wote na tutaweza kugundua ni changamoto zipi wanazokumbana nazo watoto wetu na siku hiyo kwa aliye na uwezo ataweza kuwasaidia watoto hao" alisema Nisha.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot