TRL kuwasaka wahujumu miundo mbinu - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, June 17, 2016

TRL kuwasaka wahujumu miundo mbinu

Moja ya Treni za Kampuni ya TRL waliotangaza kuanza kuwasaka wahujumu miundombinu yao.Picha na Mtandao

Na Rose Itono

KAMPUNI ya Reli Tanzania (TRL) kwa kushirikiana na Kikosi chake cha Polisi kimeanza oparesheni maalumu kwa mafundi ujenzi katika maeneo mbalimbali nchini ili kubaini wanaohujumu miundombinu ya reli na kuwapata wezi wa kokoto maalumu zinazotandazwa kwenye njia ya reli.

Pia imetoa wito kwa wananchi na hasa wanaoishi kandokando ya reli ya Ubungo Maziwa kujiepusha na vitendo vya kuhujumu tuta za reli  kwa kufungua nati kwa lengo la kusababisha ajali badala yake watoe ushirikiano kwa vyombo vya dola ili hatua zaidi zichukuliwe dhidi yao.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kukagua miundombinu ya reli Dar es Salaam jana Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Masanja Kadogosa alisema kuwa, kuna baadhi ya watu wamekuwa wakihujumu miundombinu hiyo kwa kuiba kokoto maalumu ambazo zinatandazwa kwenye njia ya reli na kwenda kuziuza.

Alisema zoezi la kumwaga kokoto katika njia ya reli imetokana na baadhi ya maombi ya wananchi waliopo kandokando ya njia hiyo ambao wamekuwa wakidhulika kwa vumbi na kwamba ni wajibu wa kila mtu kuhakikisha unalinda.

"Ukarabati wa reli hiyo kuanzia Stesheni na kumalizikia Ubungo Maziwa kwa kumwaga kokoto na unafanywa na wahandisi na mafundi wa kampuni hiyo kupitia treni maalumu ya kihandisi na kwamba utagharimu jumla ya Sh milioni 700 kukamilika",alisema Kadogosa

Aidha aliwataka wananchi kuonesha ushirikiano katika hili kwa kutoa taarifa mara tu mtu yeyote ataonekana kuchota kokoto hizo na kwenda kuziuza.

Naye Kamanda wa Kikosi cha Reli Kamishna Msiadizi Mwandamizi wa Polisi Mhandisi Simeon Chillery aliwataka wananchi kutii sheria biula shuruti kwa kuonesha ushirikiano wa kutosha kwa Jeshi hilo ili kuwabaini wote wanaohujumu miundombinu hiyo.

"Tayari vyombo vya dola tumeanza uchunguzi kujua waliofanya hujuma hiyo  ili wakamatwe kufikishwa mbele za sheria na kwamba ",alisisitiza.

Alisema yeyote atakayebainika kuhujumu miundombinu hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake huku akiwasisitiza wananchi kushirikiana na polisi ili kuwabaini wote wenye tabia kama hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot