Wasomi waitaka Serikali ya JPM kufuata sheria - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, June 17, 2016

Wasomi waitaka Serikali ya JPM kufuata sheria

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Picha na Mtandao.

David John na Carlos Nichombe

WASOMI mbalimbali nchini wamesema kuwa ni vema viongozi waliopewa dhamana ya kuwaongoza watu kufanya maamuzi yao kwa kufuata sheria na Katiba iliyopo na si vinginevyo.

Wamesema kuwa kuna maamuzi mengi yanayofanyika ni ya kukandamizaji ambayo yanafanywa tena yakiwa hayazingatii sheria mbali na kuwepo kwa katiba ambayo imeelekeza lakini imekuwa ikisiginwa na kufanya mambo kinyume na taratibu
za Nchini.

Wasomi hao wameyasema hayo Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya  mwendelezo wa Kongamano la utumiaji wa urathi wa Mwalimu Julius Nyerere katika Medani ya Siasa ya vyama vingi,ambapo ilikwenda sambamba na uzinduzi wa Kitabu cha Isha tatu za Mwalimu.

Akichangia mada katika kongamano hilo ambalo lilifanyika katika ukumbi wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Bi,Helen Kijo Bisimba aliwataka viongozi wa Serikali kuheshimu utawala wa sheria na kuzingatia misingi ya haki za binadamu.

Alisema kuwa kuna mambo ambayo yamekuwa yakifanywa ndani ya Serikali  hayazingatii Haki za binadamu,wala sheria za nchini zilizopo kwa mujibu wa katiba, huku akitolea mfano suala la kutumbua majipu ambalo linaongozwa na Rais Dkt. John Magufuli.

"kwakweli kuna ukandamizaji mkubwa ambao unaendelea lakini tukisema tunaambiwa ni majipu japo mimi sio jipo,hivyo lazima nchi iendeshwe kwa utaratibu wa kulinda haki za binadamu ikiwa pamoja na kuheshimu sheria."alisema

Tunaheshimu kazi kubwa anayoifanya Rais Dkt.Magufuli na inalengo la kusaidia taifa katika nyanja mbalimbali ambazo zilikuwa zinamatatizo hapa nchini, lakini pamoja na kazi hizo nzuri zinazofanywa na rais ni vema pia zikaheshimu misingi ya sheria na kulinda haki za binadamu hata suala la kutumbua majipu linatakiwa lizingatie sheria."alisema

"Katiba na sheria za nchi zinasema mtu aliyethibitishwa na mahakama kwa kosa fulani ndio inatakiwa kufuatwa lakini tunaona wanaotumbuliwa majipu waliwengi hawajathibitishwa na mahakama jambo ambalo linaleta shida katika ustawi wa kuheshi utawala wa sheria."alisema

Naye profesa Issa Shevji ambaye ndiye alikuwa Mwenyekiti wa  kongamano la kavazi la Mwalimu nyerere alisema katika kuendesha nchi viongozi na wananchi wanatakiwa kufuata misingi ya katiba pasipo kuangalia udhaifu au uhimara wa katiba husika ambayo hutumika kuliongoza taifa hilo.

Aidha alisema kuwa kinachofanyika katika Serikali ya awamu ya tano ni kutawala kiholela ambako kuna sababisha hofu kwa wananchi pamoja na viongozi wa chini kutokana na kuogopa maamuzi yanayoweza kuchukuliwa na viongozi wa juu pindi wanapoonekana kukosea katika utendaji wao.

"Jamii ikipata uwoga wa kutawaliwa kiholela matokeo yake ni kuanza kutawaliwa upya ambako tulikwisha ondoka huko tangu enzi za Mwalimu Nyerere kwa sababu wananchi pamoja na viongozi wa chini watakua wakijishitukia katika ambayo wanatenda kila siku" alisema Prof. Shivji.

Kwaupande wake Profesa Daud Mukangala alisema katika kuzingatia utawala wa sheria vyama vya upinzani vilianzisha harakati  za kudai utawala bora siku nyingi lakini mbali na kufanya hivyo bado kumekuwepo na changamoto na ndio maana utumbuaji wa majipu hakufuati katiba.

Alisema kuwa Katiba inapungufu na hususani katika madaraka ya rais kutokana na hali hiyo imempa mamlaka makubwa yakuweza kufanya kazi na ndio maana leo hii watu wanafukuzwa kazi kiholela.

Aidha akizungumzia kuingiliwa kwa majukumu ya Bunge alisema kuwa hata suala la kubadili matumizi kwa fedha kimsingi zinatakiwa kwanza zirudishwe Hazina na baadaye Bunge lijulishwe  ndio maamuzi mengine yanafanyika jambo ambalo kwasasa rais anamaamuzi ya kufanya vyovyote kinyume na katiba inavyoelekeza.

Aliyewahi kuwa Waziri mkuu katika Serikali ya awamu ya pili ya mzee Ally Hassan Mwinyi, Dkt. Salim Salim aliwataka wananchi  bila kujali itakadi ya vyama vyao na kutoingiza siasa na dini kuungana kwa pamoja katika kujenga ustawi na umoja wa taifa ulioachwa na baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Alisema katika insha alizoandika Mwalimu nyerere alionyesha wazi kuwa watu wote ni sawa,kufanya kazi pamoja,na jamii kuwa na umoja katika mambo yao wanayoyatenda kwa maana kufanya mambo kwa kushirikiana.

"Kimsingi ili taifa liweze kukuwa na kustawi katika njia inayotakiwa ni lazima watu waache uhasama walionao unaosababishwa na masuala mbalimbali na badala yake waungane  pamoja ili kuweza kulitumikia taifa na kwa kufanya hivyo kutaweza kuiweka nchi yetu katika mazingira mazuri ya kukua na kujitegemea" alisema.

Aidha Dkt. Salim alisema kukuwa kwa demokrasia sio kitendo cha kukurupuka bali kinahitaji kwenda polepole kulingana na hali ya nchi husika hivyo, kuwataka wale wanaotaka kutumia nguvu kukuza demokrasia wawe na subra kwani suala hilo haliitaji kutumia nguvu ya aina yoyote.

Kwa upande wao vijana waliokuwa wameshiriki kavani ya kongamano hilo walisema kuwa taifa lazima liwe na mambo mawili ,kwa maana dira ambayo inaonesha wapi tunakwenda pamoja na mtazamo kwa maana ya maono lakini kama mambo hayo yatakosekana ni dhahiri kwamba nchi itaendelea kurudi nyuma.

Pia wengine wakizungumzi uhuru wa kujieleza walisema kuwa viongozi wa Serikali wamekuwa wakifinya uhuru huo na ndio maana imefika hatua hivi sasa wanaona hata Bunge likiminywa kuonekana moja kwamoja ili wananchi waweze kufuatia kinachoendelea.

Naye Vennace mkazi wa kivule alitoa maoni yake kwamba wasomi wasitumie muda wao mwingi katika kulumbana badala yake watumie rasilimali fedha wanazopata kutoka kwa wahisani kuzunguka nchi nzima kwa lengo la kutoa elimu juu ya Katiba na sheria mbalimbali zinazotumika nchini ili kuwajengea uelewa mpana wananchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot