Na mwandishi wetu.
![]() |
| Shamba la mahindi lililopo huko Kijiji Cha Nkali Nyasa Mkoani Ruvuma |
TAKWIMU zinaonyesha kuwa kilimo ndio kinatoa ajira kwa wananchi wengi na kuchangia pato la Taifa , ambapo zaidi ya asilimia 77 ya Watanzania wamejiajiri kwenye sekta hiyo lakini hawakopesheki kwa sababu wengi wao hawakidhi masharti ya wakopeshaji.
Pia Mkopaji hutakiwa kuwa na dhamana za mali zisizohamishika hati za viwanja na masharti mengine ni mambo ambayo yamekuwa na mchango mkubwa kwa wakulima kushindwa kumudu kupata mikopo hiyo.
Vile vile ardhi ya vijijini inaonekana kuwa haina thamani hivyo siyo kazi rahisi kuuzika kirahisi pale mkopaji anaposhindwa kulipa, na pia riba kubwa ni changamoto nyingine inayowakabili wakulima na mbaya zaidi kukosekana kwa uhakika wa mavuno kutokana na utegemezi wa mvua ambazo hazina uhakika kunawaweka pagumu zaidi.
Pia,bei duni ya mazao ya kilimo, mabadiliko ya hali ya hewa na ukosefu wa mikopo kwa wakulima hususan wadogo wadogo zimefanya sekta hiyo kuwa duni na vijana wengi kuikimbia kana kwamba sio sekta yenye faida.
Akizungumza hivi karibuni Mkurugenzi wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo nchini(PASS) Nicomed Bohay anasema wako kwa ajili ya kutoa dhamana kwa wakulima ambao hawakopesheki na Benki.
Anasema kuwa mfumo wa PASS jukumu kubwa lake ni kufadhili wakulima na kuhakikisha uwekezaji mkubwa unafanyika kwa wakulima wadogo ili kuleta tija.
Anasema PASS ni chombo kilichoanzishwa mwaka 2000 ilikuchochea uwekezaji na kukuza kilimo cha biashara nasekta zinazohusika.
pia anasema Ilisajiliwa mwaka 2007 kama Asasiisiyokuwa ya Serikali kwa mujibu wa Sheria ya Ushirikishaji Wadhamini ya mwaka 2002 dira ikiwa ni kuwa asasi inayoongoza katika utoaji wa huduma za fedha na maendeleo ya biashara katika sekta ya kilimo.
Vile vile anasema Asasi ya PASS inawajibika katika utoaji wa huduma za maendeleo ya kilimo cha biashara na fedha kwa wafanyabiashara wajasiriamali wadogo na wa kati kuwaunganisha katika taasisi za fedha.
Anasema huduma zinazotolewa na PASS ni huduma za fedha za Maendeleo ya Biashara za PASS kwa wateja kwa kuchangia gharama. Huduma hizo ni pamoja na: Upembuzi yakinifu Kuandaa mipango ya biashara
Pia kujenga uwezo mfano katika maeneo maalumu yakitaalamu na kuwanganisha wakulima katika vikundi ambavyo vinaweza kutumika kama vikundi maalumu kwaajili ya kilimo cha mkataba, kusambaza pembejeo
kwa mkopo, kufanya mazungumzo ya bei na kutoahuduma ya ushauri.
Anasema fedha zinazotolewa na PASS ziko chini ya mpango wa mnyororo wa thamani ikiwa ni pamoja na kununua mazao ya wakulima hao waliokopeshwa.
Mazao hayo yamewekwa kwenye maeneo 14 na kwamba eneo la kwanza ni mazao ya nafaka ambayo ni mahindi na mpunga, mazao ya mafuta kama vile alizeti na ufuta, kilimo cha miwa kwa ajili ya sukari, korosho na mazao ya wanyama, nyama na maziwa.
Vile vile mengine ni ufugaji wa kuku na samaki, nyuki na mazao yake kama vile asali na kilimo cha mboga Benki hiyo imeanza kuwakopesha wakulima wadogowadogo pekee kwani ndio kundi ambalo halipati mikopo kirahisi kwenye taasisi za fedha na nia ya serikali ni kusaidia wakulima hao ambao ndio wengi nchini ili waweze kulima kwa tija na kukuza uchumi
Pia anasema kuwa wakulima wanakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji wadau kuzitatua ili waweze kunufaika na wanachokifanya badala ya kuwa kama ilivyo sasa katika maeneo mengi.
Bohay anasema kuwa PASS wameweza kutoa dhamana ya zaidi ya bilioni 315 kwa vikundi laki 3230,000 vya wakulima na wafanyabiashara na wafugaji mbalimbali hapa nchini.
Anasema tangu asasi hiyo ianze mwaka 2000 wameweza kutoa dhamana kwa wakulima na wafugaji mbalimbali na hawajapata hasara kubwa kama mabenki mengi yanavyoogopa kuwekeza kwenye kilimo.
Pia anasema hasara ambayo wamepata tangu waanze kutoa dhamana ni jumla ya bilioni 5 ambayo ilitokana na kuweka dhamana kwa wakulima kutokana na mabadiliko ya tabia nchi ndiyo yakaathiri uchumi kwa kiasi kikubwa hivyo hasara hiyo ni sawa na asilimia 1.5 ya dhamana waliyotoa.
Vile vile anasema kuwekeza kwenye sekta ya kilimo siyo hasara bali kinachotokea ni kuelewa vizuri sekta hiyo na kuhamasisha walime kibiashara.
Anasema kwa mwaka jana PASS imetoa dhamana ya bilioni 56 kwa wakulima na wafugaji hii ni kutokana na mahitaji kuwa makubwa zaidi.
Anasema PASS inasaidia wakulima kuandika michanganuo au kikundi kwa utaalamu zaidi na kuwasilisha benki za biashara ili waweze kupatiwa mikopo.
Anasema asilimia 99 ya michanganuo yote wanayoandika inapitishwa na benki na wanatoa dhamana kuanzia asilimia 30 hadi 60 na kwa vikundi vya wanawake asilimia 80.
Bohay anasema taasisi za kifedha zinatakiwa kuchangamkia fursa ya kutoa fedha katika sekta ya kilimo ili kukuza kibiashara na kupata wateja wengi.
Pia aliwataka wakulima kutumia mbegu bora na kutumia pembejeo zenye tija ili kupunguza hasara kwao na kutumia mbegu za muda mfupi ambazo zinahimili ukame.
Vile vile anasema wakulima wanakabiliwa na chngamoto mbalimbali moja ikiwa ni wakulima kukosa hati za ardhi hivyo kukosa kukopesheka na benki.
Anasema pamoja na umuhimu wa Sekta ya Kilimo, bado ukuaji wa sekta hiyo umekuwa ukikabiliwa na changamoto mbali mbali kama vile kiwango kidogo cha uzalishaji ufinyu wa upatikanaji wa fedha za mikopo kwa ajili ya kuendeleza kilimo nchini.
Anasema serikali ilitakuwa kuangalia kwa umakini suala hilo ili kutoa hati za ardhi ambazo wakulima wengi wanaweza kukopeshwa na mabenki.
Hata hivyo anasema baadhi ya benki zimeanza kukubali hati za kimila zinazotolewa na wakulima ili kupata mkopo kutoka benki ili kuendeleza sekta hiyo.
Anasema elimu inatakiwa itolewe kwa wakulima na wafugaji pamoja na ushauri ni mbegu gani wanatakiwa kutumia katika kulima kibiashara.
Anasema kuongea na wadau mbalimbali nje ya nchi waweze kuanziasha bima ya wakulima ili iwe kama sekta nyingine ambazo kama mazao yakikauka na ukame waweze kulipwa fidia.
Bohay anasema hatua ya udhamini wa mkopobaada ya benki kumkubali mteja pamoja na mpango wa
biashara wa PASS, kutakuwa na mawasiliano zaidi kati ya Mwongozo wa pass
Anasema PASS na benki watakubaliana kuhusu kiasicha udhamini wa mkopo PASS itatoa Hati ya Udhamini wa Mkopo katika Makao Makuu ya benki na hatua ya Utoaji wa Mkopo.
Anasema Benki itatoa mkopo na utaratibu wa urejeshaji pamoja na mapendekezo ya utaratibu wa kutoa mkopo kama ilivyo katika Mpango wa Biashara iliyoandaliwa naPASS.
Pia anasema hatua inayofuata baada ya Utoaji MkopoBenki itafuatilia utaratibu wa marejesho na
kutembelea mteja mara kwa mara na itakapowezekana watakuwa na mwakilishi wa PASS
Vile vile anasema Benki itatoa taarifa kwa PASS kuhusu mabadiliko yoyote makubwa yanayoathiri urejeshaji wa mkopo wa mteja hili litahusisha mapendekezo ya utaratibu mpya wa urejeshaji mkopo na kupanga upya itakapolazimika
Anasema Kama mteja ameshindwa kurejesha mkopo, benki watamtembelea mteja mara kadhaa kulazimisha
urejeshaji wa mkopo. Hatua za ziada za kumrekebisha mteja zitatolewa kwa makubaliano kati ya PASS na benki inapobidi.
Hata kama jitihada zote zimeshindwa dhamana ya mkopo itauzwa kufuatana na makubaliano ya mkopo yaliyofanywa kati ya benki na PASS.



No comments:
Post a Comment