Simbachawene awatoa hofu wananchi shida ya sukari - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, June 17, 2016

Simbachawene awatoa hofu wananchi shida ya sukari

Viroba vya sukari vikiwa stoo tayari kwa kwenda kuuzwa

Na Goodluck Hongo

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene amewata wananchi kuvuta subira wakati Serikali ikiendelea kushughulikia suala la sukari.

Simbachawene alitoa kauli hiyo Dar es Salaam jana baada ya kuulizwa na wananchi juu ya kupanda kwa bei ya sukari wakati alipofanya ukaguzi wa mradi wa mabasi yaendayo kasi na kisha kutembelea baadhi ya maduka ya Kariakoo.

Alisema muda si mrefu sukari itarudi katika hali yake ya kawaida kwa kuwa Serikali inandelea na utaratibu wa kuhakikisha kuwa bidhaa hiyo inapatikana kwa wingi na kubaki katika bei yake ya kawaida.

Akizungumzia kuhusu mradi wa mabasi ya mwendo kasi,Simbawene alisema ni lazima watanzania waishi kwa kufuata sheria ikiwemo za usalama barabarani kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia zaidi kuharakisha maendeleo

"Nimekagua mradi huu kwani nimetumia dakika 10 kutoka Kimara hadi Gerezani kwani kila kituo basi lilikuwa linasimama hivyo huu ni mradi mkubwa lakini changamoto bado zipo hasa kwa watumizi ya barabara hizo"alisema Simbachawene

Alisema kila mtu lazima afuate sheria lakini pia hata wafanyabishara wadogo lazima waondelewe katika maeneo ya jiji ili kuweka mji wetu katika hali ya usafi wakiwemo ombaomba ambao wengine wanatumia kama ATM.

"Nakuagiza RC kuwaondoa wafanyabishara wote katika maeneo wasiohusika ikiwemo hata kule posta kwani hatuwezi kuwapenda Vijana wenye nguvu kwa kuwaruhusu wauze leo au big G bali ni lazima tutafute mbinu za kuwasaidia lakini utumie Kamati ya Ulinzi na Usalama kuweka askari masaa 24 ili kulifanya jiji liwe safi.

Akizungumzia kuhusu mradi wa pili wa mabasi yaendayo kasi,alisema mradi huo uko mbioni kuanza na safari hii utaanzia barabara ya kilwa na kutakuwa na madaraja ya juu ya magari (flyover) mbili za Chang'ombe na Uhasibu ikiwemo kujenga barabara zote za mitaa katika jiji la Dar es Salaam.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda alisema yeye na timu yake tayari wanaendelea na oparasheni ya kuwaondoa ombaomba na wafanyabiashara wadogo katika maeneo wasiohitajika.

"Kwa sasa jiji la Dar es Salaam lina wakazi milioni tano hivyo mikakati ya kulifanya jiji kuwa katika hali ya usafi inaendelea lakini pia tumeona wafanyabiashara hasa wale wa maduka makubwa wauze hadi saa nne usiku"alisema Makonda

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot