![]() |
| Mfano wa madawati yaliyokabidhiwa kwa mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda |
Na Goodluck Hongo
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepokea madawati 60 yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni tisa kwa ajili ya shule ya Msingi Miembeni iliyopoa Vingunguti jijini Dar ES Salaam.
Madawati hayo yalikabishiwa jana katika shule hiyo na Mwakilishi wa Shirika la Youth Welfare Trust Vipul Vithilan ambaye alisema bado kuna mdawati mengine 30 kwa ajili ya shule hiyo ambayo bado hajakamilika.
Akizungumza mara baada ya kupokea madawati hayo,Makonda alisema ni lazima wanafunzi hao wasome kwa bidii ili waweze kuja kuwa wanasayansi
Alisema kupatikana kwa madawati hayo ni wazi kuwa kuna watu wengine wamejinyima na ili kutoa fursa kwa wanafunzi mhao kukaa katika madawati hivyo ni wajibu wa wanafunzi kusoma kwa bidii
"Natoa sh.50,000 kwa kila mtoto ambaye amejiamini na kutoka mbele bila kuogopa kwani huwezi kufaulu vizuru kama mwanafunzi anakuwa muoga lakini pia nawataka msome sana hasa masomo ya sayansi"alisema Makonda
Kwa upande wake Naibu Meya wa Manispaa ya Ilala Omar Kumbilamoto alisema wao watandelea kutafuta wahisani ili kutatua kero za wananchi wa Vingunguti
Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Ailika Yahaya alisema shule hiyo ilinzishwa mwaka 2002 na inawafunzi 2165 na walimu 49 kati yao wanaume wakiwa wanne
"Tunashukuru sana kupata msaada huu kwani utawawezesha wanafunzi wengi kukaa katika madawati hivyo tunawaomba na wahisani wengine kutusaidia katika mahitaji ya shule kama ilivyo madawati"alisema Yahaya



No comments:
Post a Comment