![]() |
| Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo, Nape Nnauye |
WAZIRI wa Habari,Utamaduni,Michezo na Sanaa Nape Nnauye ameahidi kuyafungia maduka yote yaliyopewa vibali vya kufanya biashara ya vinyago vya ndani ya nchi na sio kuuza vya nje ya nchi.
Kauli hiyo aliitoa Dar Es salaam jana wakati alipokuwa akizungumza na wasanii wa uchongaji vinyago alipotembelea eneo hilo kujua changamoto zinazowakabili.
Alisema Serikali imetoa vibali kwa wafanyabiashara kuanzisha maduka hayo ili kuweza kuwasaidia wasanii wa uchongaji wa vinyago katika kupata masoko ya uuzaji wa kazi zao.
"Serikali imetambua changamoto zenu zinazowakabili na ndio maana imewapatia wafanyabiashara vibali vya kunua na kuuza,lengo ikiwa ni kapambana na katika sekta ya masoko ya biashara ya vinyago nchini" alisema Nape.
Nape alisema kuwa Serikali inampango wa kuifanya Sekta ya uchongaji kuwa rasmi hivyo kuahidi kushughulikia changamoto zinazoikabili sekta hiyo ili iweze kuwasaidia wasanii katika kupata kipato pamoja na kukuza uchumi wa nchi.
Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Tanzania(TAFCA), Adrian Nyangamalle aliiomba Serikali kuwapatia hati milki ya kiwanja hicho ili waweze kujenga majengo na masoko yatakaypwawezesha kufanya kazi zao.
Aliongeza kuwa mlundikano wa kodi unaotozwa na Serikali kwa wafanyabiashara hao umeweza kushusha mauzo ya vinyago vyao toka asilimia 50 hadi 15 na kuitaka Serikali kupunguza kodi hizo ili kuweza kuwavutia zaidi wateja wa nje katika kununua bidhaa hizo.
"Mauzo yetu yameshuka kutokana na wateja wetu wakubwa ni wa kutoka nje ya nchi hivyo kutozwa kwa kiwango kikubwa cha kodi kumesababisha wateja hao kuacha kununua bidhaa zetu na tumejikuta tukikosa kabisa mapato" alisema Nyamangalle.



No comments:
Post a Comment