![]() |
| Malkia wa Mipasho nchini, Khadija Kopa |
MALKIA wa mipasho nchini, Khadija Kopa amefunguka na kusema kuna ubaya pale mwanamke mwenye umri mkubwa kutoka kimapenzi na mtoto chini ya miaka 18, ila kijana akishavuka umri huo hakuna cha kushangaza.
Kopa alifunguka kuwa haoni ajabu wanawake wenye umri mkubwa kutoka kimapenzi na vijana wadogo, ilimradi kuna mapenzi ya dhati kati yao.
Malkia huyo alisema kuwa mapenzi ni maridhiano, hayachagui umri na hufanana mno na majani yanayoweza kuota mahali popote.
“Huwa nawashangaa watu wanaosema mapenzi ya namna hiyo ni ajabu, kama kuna maridhiano baina yao uajabu wao unatoka wapi? Waache kufuatilia yasiyowahusu kama wenyewe wanapendana iweje wewe utie maneno,” alipasha Kopa.



Hapo umenena mamaaaaaaaaaaaaaaa
ReplyDeleteXema malkia wa Mipasho jaribu basi hata kuchagua watuwa rika lako kidogo usichukue watoto wadogo tu
ReplyDelete