Mkondya aaga Dar - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 16, 2016

Mkondya aaga Dar



Mkuu wa Oparesheni Kanda Maalum Ilala,Lucas Mkondya, (kushoto) akiwasili wakati wa ziara ya utambulisho wa kamanda wa mkoa wa Ilala,Salum  Hamduni,(katikati) Polisi Ufundi Dar es Salaam jana.Picha na Heri Shaaban
Na Heri Shaaban

JESHI la Polisi limewataka Polisi wake kufanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi na misingi yake pamoja na  kutumia lugha nzuri kwa wateja wao.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana, na Mkuu wa Oparesheni Kanda Maalum Ilala,Lucas Mkondya,wakati wa kuwaaga polisi wake aliofanya nao kazi na kuwakabidhi kwa Kamanda mpya wa Ilala,Salum Hamduni.

"Nawaomba vijana wangu wa Ilala ambao nimefanya nao kazi ushirikiano wenu ambao mlikuwa mkionyesha kwangu nawaomba mumpe kamanda mpya ambaye leo nimewatambilisha rasmi huku mkizingatia maadili ya
kazi"alisema Mkondya.

Alisema kwa sasa mkoa wa Ilala upo salama na wasifanye kazi kwa mazoea yale ya awali kila kiongozi na mipaka yake hivyo wafanye kazi yao kwa kufuata misingi ya taaluma bila kukiuka miiko yake.

Aliwataka askari hao wawe na nidhamu ya kazi kila mmoja kwa kutekeleza  kauli mbiu ya Serikali hapa kazi tuu ili waweze kufikia malengo ya jeshi la Polisi.

Amemtaka kamanda wa Ilala kushirikiana na mkuu wa trafiki mkoa wa Ilala katika kupunguza ajali za kizembe baada kuonekana Ilala ndio Kinara wa ajali za barabarani Dar es Salaam na wilaya ya Ukonga na
Buguruni ndio zinapotokea kwa kuwa na idadi kubwa ya watu.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala,Salum Hamdun,aliwataka askali wote wa Ilala kufanya kazi kila mmoja kwa wajibu wake na nafasi yake .

Salumu alisema Ilala ina askali jumla 2500 pamoja na maofisa wake wa polisi ambao wanafanya kazi na kutekeleza majumu ya kazi kwa kufuata misingi mema ametaka waendelee kutekeleza wajibu wao..

Aliwataka wakuu wa vituo vya Polisi wote kila mmoja kufunya kazi na mpango mkakati wa jeshi la polisi walivyopangiwa bila kuzembea wakatumbuliwa jipu kwa utendaji wao mbovu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot