Benki ya Amana Yatoa Elimu Dar - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 16, 2016

Benki ya Amana Yatoa Elimu Dar

Na Irene Clemence

BENKI ya Kiislamu ya Amana imewapa mafunzo ya namna ya uendeshaji wa shughuli za kibenki kwa wanafunzi wa shule ya msingi upanga ili waweze kukua wakijua shughuli zinazofanywa na benki hiyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari  Dar es salaam jana Kaimu Meneja wa Benki hiyo tawi la Posta Nashir Mwano alisema kuwa,uongozi wa Benki hiyo umeamua kuitumia nafasi hiyo kama njia mojawapo ya kushiriki na watoto katika maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika.

Alisema ni wajibu wa msingi kwa watoto kukua huku wakijua namna shughuli za kibenki zinavyoendeshwa na kusisitiza kuwa kufanya hivyo kunawajenga watoto kukua wakifahamu shughuli mbalimbali zianzofanywa
na Taasisi za  Kifedha ikiwemo Benki ya Amana.

Aidha aliongeza sababu nyingine ya Benki hiyo kukutana na wanafunzi hao ni kutoa mchango wao kwa serikali katika jitihada zake za kutoa elimu.

"Tumetambua umuhimu  wa watoto nchini na duniani kwa ujumla benki yetu imeamua kuungana nao katika sikukuu hii ambayo ni ya pekee kwao kutambua haki zao za msingi"alisema Nashir

Aliongeza kuwa benki hiyo imekuwa ikitoa misaada mbalimbali kupitia mfuko wa msaada katika vituo vya kulelea watoto yatima na wenye shida kupitia mfuko wa msaada wa benki  ili waweze kutambua kuwa jamii
inawakumbuka.

Kwa upande wake Mwalimu wa hisabati Shule ya Msingi Upanga Agnether Manjoli alisema kuwa wamefurahi sana kwa Benki hiyo kuutambua umuhimu wao kwani watoto wamepata elimu mbalimbali kuhusiana na masuala ya kibenki na kuwataka watoto kuitumia elimu waliyoipata kwa kuwaelimisha wenzao.

Aliwataka wazazi kuwa karibu na walimu kwa kufuatilia mienendo yao shuleni kwani kwa kufanya hivyo kutawezesha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.

Aidha aliitaka serikali kuangalia namna ya kuiboresha sheria ya watoto ili iweze kuendana na wakati na kuwezesha kizazi kijacho kukua katika misingi inayofaa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot