Kanda ya Ziwa,Pwani yaongoza Maambukizi sikoseli - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, June 16, 2016

Kanda ya Ziwa,Pwani yaongoza Maambukizi sikoseli


Mbu Jike
Heri Shaaban na Irene  Clemence

IMEELEZWA kuwa  mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Pwani imeongoza kuwa na wagonjwa wa selimundu (Siko Seli)kutokana na maeneo hayo kuwa na mazalio ya Mmbu wanaoneza ugonjwa wa Malaria.

Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana, na Mratibu wa Kitengo cha Sikoseli katika Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili(MUHAS)Dkt. Deogratias Soka wakati wa kuzungumza na waandishi wa habari
kuelezea maadhimisho ya siku hiyo juni 16 mwaka huu.

Dkt.Soka alisema maeneo hayo ya ukanda wa Pwani na Kanda ziwa yamekuwa na mazalio wengi hivyo ndio imekuwa sababu ya mikoa hiyo kuwa na wagonjwa hao.

"Maeneo ya kanda ya ziwa na Pwani yamekuwa na uhusiano mkubwa na ugonjwa wa malaria hivyo kupelekea kupata vinasaba vya ugonjwa wa sikoseli"alisema Dkt Soka.

Alisema madhimisho hayo mwaka huu yanafanyika Dar es Salaam  ambapo mgeni rasmi Naibu Waziri wa
Wizara ya  Afya Dkt.Hamisi Kigwangwala ndio atakayepamba sherehe hizo.

Aidha alisema utafiti umeonesha asilimia 15 ya Watanzania wana vinasaba vya sikoseli hivyo inamanisha kuwa watu wote wenye sikoseli uwezo wa kupata watoto wenye ugonjwa huo.

Alisema kupitia siku hiyo kabla kuitimisha kwake watatoa elimu kwa umma katika kuelewa madhara ya
ugonjwa huo na kujikinga kwake.

Dkt.Soka alisema siku hiyo Duniani  kwa kutambua athari kubwa zinazotolewa  na ugonjwa huo Tanzania
wanadhimisha siku hiyo kupitia matukio mawili muhimu ambapo alisema tukio la kwanza litafanyika bagamoyo la mdahalo wa wazi na Makumbusho ya taifa katika kutoa elimu.

"Tanzania ni nchi ya tano Duniani kwa watu wenye sikoseli hivyo athari kubwa sana katika jamii
kupata uelewa zaidi kwa ugonjwa huu utasaidia kuzuia vifo visivyo vya lazima kutokana na ugonjwa
huo .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot