LAPF yatoa onyo kwa maofisa Utumishi - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 21, 2016

LAPF yatoa onyo kwa maofisa Utumishi


Na Carlos Nichombe

Maofisa Utimishi nchini wametakiwa kuwapatia uhuru wafanyakazi wa kuchagua mifuko ya hifadhi ya kijamii wanayotaka kujiunga.

Hayo yalisemwa Dar es salaam na Meneja Mkuu wa masoko na Uhusiano wa mfuko wa hifadhi ya kijamii wa LAPF, James Mlowe wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ilivyo kwenye mifuko ya hifadhi za kijamii hapa nchini.

Alisema kuwa kitendo cha maafisa utumishi kuwalazimisha wafanyakazi kujiunga katika mifuko waitakayo wao ni kinyume na sheria za nchi hivyo maofisa hao wanapaswa kuchukuliwa hatua kutokana na kosa hilo.

"Zipo baadhi ya taasisi ambazo mfanyakazi akienda kusaini mkataba wa kufanya kazi huwa wanawapatia na fomu za kujiunga na mifuko ya hifadhi ya kijamii ambayo wao hata hawajawahi kuulizwa kama wataka kujiunga au sio, kwahiyo maofisa hao wachukuliwe hatua kali za kisheria zitakazo weza kukomesha vutendo hivyo ambavyo vimeonekana kuongezeka kwa kasi hapa nchini" alisema.

Mlowe alisema kila mfanyakazi anauhuru wa kuchagua mfuko anaohitaji kujiunga na pindi waonapo maofisa utumishi wakiwalazimisha kujiunga katika mifuko ya hifadhi ya jamii wasiyoitaka wao waweze kuwaripoti katika vyombo vya kisheria na hatua mbali mbali ziweze kuchukuliwa dhidi yao.

Akizungumzia kuhusu deni wanaloidai Serikali Mlowe alisema wamefanya makubalioano mbalimbali ambayo yataiwezesha serikali kulipa fedha hizo kwa wakati ili ziweze kuwekwezwa katika mambo mengine ambayo yataisaidia nchi katika ukuaji wake wa maendeleo.

Alisema kuwa mfuko huo umeweza kuwekeza kwenye ujenzi wa majengo mbali mbali ikiwemo vyuo vya afya ambavyo vinazalisha wataalamu wa afya na watakaoisaidia jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot