![]() |
| Mojawapo ya majengo yaliyobuniwa na Baraza hilo. |
Na Rose Itono
BARAZA la wafanyakazi wa Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) limechagua Msajili wa Bodi hiyo Mbunifu Jehad Jehad kuwa, Mwenyekiti mpya wa baraza hilo.
Pia limemchagua Jesca Kaseka kuwa Katibu wa baraza hilo akisaidiwa na Mashaka Fulano.
Akizungumza Dar es Salaam jana mara baada ya baraza hilo kuzinduliwa rasmi hivi karibuni Msajili ambaye pia ni Mwenyekiti mpya wa baraza hilo Mbunifu Jehad alisema kuwa, lengo kubwa la mabaraza mahali pa kazi ni kuweza kusaidia bodi kufanya kazi kwa weledi ili kuleta ufanisi.
Aidha aliyataja madhumuni mengine ya mabaraza kuwa ni pamoja na uwepo wa ushirikishwaji wa wafanyakazi mahali pa kazi na ni wajibu wa mwajiri kuunda Baraza la wafanyakazi na hii ni kwa mujibu wa sheria ya ajira na mahusiano kazini Namba 6 ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2007.
Hivi karibuni Bodi ya Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB) ilizindua Baraza la Wafanyakazi na kuwataka wajumbe wa baraza hilo kutatua kero za wafanyakazi ili kuleta ufanisi katika utendaji wa bodi.
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt.Ambwene Mwakyusa aliwaasa wajumbe wa baraza hilo kulitumia vizuri ili
kutatua kero za wafanyakazi na hatimaye kuleta ufanisi katika utendaji wa Bodi.
Dkt. Mwakyusa aliwasisitiza wajumbe wa baraza hili kulitumia vizuri ili kutatua kero za wafanyakazi na hatimaye kuleta ufanisi katika utendaji wa Bodi.
"Baraza hili linaanzishwa baada ya mkataba wa kuwashirikisha wafanyakazi na kuafikiwa kati ya pande mbili ambazo ni Menejimenti ya Bodi na Chama Cha Wafanyakazi (TAMICO)",alisema na kuongeza kufanya kazi kwa weledi ili kuwa mfano wa kuingwa na mabaraza mengine.



No comments:
Post a Comment