Mwanadada anayetamba na ngoma ya Main Chick, Maua Sama amesema yeye
hategemei 'kiki' ili ku-'hit' bali uzuri wa kazi zake, na kuwataka
wasanii wengine waache kutafuta 'kiki' ili kupata majina bali wajikite
kwenye kutengeza kazi nzuri.
Akizungumza
leo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Maua amesema kuwa wasanii
wengi wamejikita kwenye kutafuta kiki badala ya kuwapa mashabiki ladha
tofauti na kusisitiza kwamba dhana ya kiki inapaswa kufutika ili kila
mtu afanye kazi nzuri.
"Ukifanya muziki mzuri
lazima tu utapata jina, wala hakuna haja ya kiki, mfano mzuri mimi hapa
ni msanii ambaye nimepata sapoti nzuri sana kwenye 'game' bila
kuongelewa kwa mambo mabaya ya kiki, 'The real deal is good music' siyo
skendo, japo mimi nina skendo ya kutoa ngoma kali siku zote".
Maua aliwaambia Dullah na Jay R watangazaji wa kipindi hicho.
Sama ameongeza kwamba katika muziki wapo
wasanii ambao wanafanya muziki mbaya lakini wanapewa nafasi kubwa ya
kusikilizwa kutokana na kiki lakini hana chuki nao kwani pia watu wa
aina hiyo wana mashabiki zao wanaopenda kuwasikiliza.
"Mimi nina wivu wa maendeleo
sana, lakini sina chuki na watu wanaofanya muziki mbaya kwani hata wao
wana masoko yao na wanauza ila kinachotokea kwangu nikimuona mtu katoa
kazi mbaya mimi naingia kutengeneza 'hits' kali ili nipate soko zaidi". aliongeza Maua.
Hata hivyo Maua ameongeza kuwa msanii
yoyote ambaye huandika nyimbo zake kipindi anapokuwa kwenye hisia yoyote
ni wazi wimbo huo ukiachiwa hewani lazima uwe mkali kwa kuwa unakuwa
umebeba uhalisia na hisia za kweli.
No comments:
Post a Comment