Nembo ya Chama Cha Mapinduzi |
Na Sekela Mwambene
VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kutanguliza mbele maslahi ya umma katika kutekeleza mambo mbalimbali kuliko yao binafsi ili kuweza kurudisha imani kwa Watanzania iliyo potea kwa Chama hicho.
Akizungumza na Blogu hii Dar es Salaam jana Mwanajeshi mstaafu wa Jeshi la anga la wanachi wa Tanzania(JWTZ),Japhet Mwandimo alisema kuwa viongozi wengi wa CCM wamesahau kufata maadili ya Chama na kujipangia taratibu zao wenyewe ikiwemo zile za kujilimbikizia mali za Umma.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi anayetarajia kumaliza muda wake, Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho katika mkutano mkuu uliofanyika mwaka jana. |
Alisema kuwa katika kuelekea kwenye uchaguzi wa viongozi wa chama hicho unaotarajiwa kufanyika Kesho mjini Dodoma,amewasa viongozi watakao chaguliwa kuishi katika maadili ya chama hicho yaliyo achwa na waasisi wa chama hicho ili kuweza kuimarika zaidi.
" Historia ya Chama hiki kilizaliwa mwaka 1977 kikiwa na Misingi Imara inayo jenga Umoja wa kitaifa kwa maana kuwa viongozi wake wasiwe mabepari, wanyanyasaji, Makabaila watwana mbele ya wananchi wanyonge pamoja na kutoiba mali zao ummalakini kwa hivi sasa viongozi hao wamesahau malengo ya uanzishwaji wa Chama hikina kujilimbikizia hadhina kubwa ya mali za umma"alisema Mwandimo.
Aliongeza kuwa Viongozi wanaobainika kufanya vitu vinavyokwenda kinyume na maadili wanapaswa kuchukuliwa hatu kali za kisheria ikiwemo kufukuzwa kazi pamoja na kufilisiwa mali zote ambazo wamezichuma kwa njia ya dhuluma.
Aidha aliwataka wanaCCM kutumia vyema nafasi waliyoipata katika uchaguzi kwa kuchagua viongozi wenye maadili mema ili kuweza kujenga umoja na mshikamano wa chama husika ambao ulivunjwa na baadhi ya viongozi wasio waadilifu kwa hulka zao binafsi za kugombania nyadhifa mbali mbali za kukiongoza Chama hicho
Mwandimo alisema Chama hicho kilikumbwa na migogoro mbali mbali mwaka jana wakati wa uchaguzi mkuu,na kusababisha kuibuka kwa makundi yaliyosababisha mpasuko mkubwa na kupelekea kutokuwepo kwa maelewano mazuri ndani ya chama hicho kikongwe hapa nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na anayetarajiwa kuwa mwenyekiti mpya wa CCM akizungumza na wanachama wa chama hicho mara baada ya kuteuliwa kugombea nafasi ya urais. |
Akizungumzia utendaji kazi wa Rais, Dkt. John Magufuli, alisema kinachofanyika kwa sasa ni kuitoa nchi mikononi mwa Wanasiasa wasio waadilifu pamoja na Wafanyabiashara waliokuwa wakijinufaisha mali za umma na kuirejesha mikononi mwa wananchi mbao ndio waamuzi wakuu.
Alisema kuwa Wanaccm wanapaswa kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na kiongozi huyo ili kuweza kuonyesha msimamo wa chama juu ya kusimamia maadili na mali ya umma.
"Wanaccm wanatakiwa kuwa ndio watu wa kwanza kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika upambanaji wa masuala ya rushwa ili kuweza kuwavuta wapinzaniambapo pia na wao wanatakiwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais huyo na sio kubeza kila kitakacho tendeka."alisema Mwandimo.
No comments:
Post a Comment