Mshambuliaji wa Timu ya Azam, John Bocco akishangilia bao katika moja ya mechi zilizochezwa katika msimu wa ligi uliopita. |
Na Mwandishi Wetu.
KUFUATIA kuzuka kwa tetesi zinazodai kocha wa timu ya Azam FC Zeben Hernandez kutokubali kiwango cha shambuliaji wa timu hiyo John Bocco, uongozi wa timu hiyo ubeibuka na kudai kuwa mwalimu huyo bado hajatoa tathmini yake.
Uongozi huo kupitia kwa katibu mkuu wake Sadi Kawemba umesema kuwa kocha huyo anatarajiwa kutoa
tathmini ya timu hiyo pindi atakapoanza rasmi kuifundisha timu hiyo Jumatatu ya wiki ijayo.
Kawemba alisema kuwa anashangazwa na taarifa hizo kwani wao kama uongozi hawajapokea taarifa zozote
kutoka kwa mwalimu inakuajna kusema kuwa watu wa nje wanaongea kitu wasichokijua.
Azam iliingia kambini mwanzoni mwa mwezi huu kwa ajili ya kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao wa
ligi kuu ikiwemo kucheza mchezo mmoja wa kirafiki kama majaribio kwa wachezaji wao waliokuja katika
majaribio.
Kuelekea msimu ujao timu hiyo imepanga kuwa na kikosi bora zaidi ili kutimiza adhma yao ya kunyakua ubingwa baada ya Yanga kutwaa taji hilo misimu miwili mfululizo.
Mshambuliaji wa Timu ya Azam John Boko, akimtoka Nadir Haroub 'Canavaro' wa Yanga katika kipute hicho moja ya mechi iliyozikutanisha timu hizo. |
Afisa habari wa timu hiyo Jaffar Idd Maganga alisema kuwa yeye ndio muhusika wa kutoa taarifa ya timu hiyo hivyo watanzania wasiymbishwe na taarifa zinazotolewa na watu wasioitakia mema timu hiyo.
"Mimi ndio muhusika mkuu wa kutoa taarifa zinazoihusu timu hii kwa hiyo hizo taarifa zinazotolewa si za kweli tumuache kocha afanye kazi yake na akimaliza ataweza kusema nani abaki katika kikosi chake na nani atoke lakini watu waache kusikiliza maneno ya uvumi yasiyo na ukweli wowote ule" alisema Maganga.
No comments:
Post a Comment