Maafisa kadha wa polisi wanahofiwa kufariki baada ya mtu mwenye silaha kushambulia kituo cha polisi eneo la Kapenguria, kaskazini magharibi mwa Kenya.
Mtu huyo anadaiwa kuvamia kituo hicho kumnusuru mshtakiwa aliyekuwa amekamatwa akishtakiwa kuhusika katika ugaidi, gazeti la Daily Nation limeripoti.
Gazeti hilo linasema huenda maafisa hadi watano wameuawa.
Ufyatulianaji wa risasi bado unaendelea.
No comments:
Post a Comment