Ni moja kati ya Barabara zunazoendelea kujengwa nchini |
WAKALA wa Barabara Nchini(TANROADS) umeitaka serikali kuwalipa fidia wananchi walioko pembezoni mwa barabara zinazotakiwa kujengwa kwa wakati ili kuweza kukamirisha miradi ya ujenzi kwa wakati.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Jijini Dar
es salaam Mhandisi wa miradi mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi Ngusa Julius
alisema miradi mingi inayoendelea hapa nchini imeshindwa kukamilika kwa wakati
huku ulipaji wa madeni unaonekana kuwa ndio kikwazo kikubwa.
Alisema
wamekuwa wakifanya jitihada kubwa kuweza kuwashinikiza serikali ili waweze
kuwalipa wananchi waliopo pembezoni mwa barabara lakini ufinyu wa bajeti
iliyokuwa ikitengwa kwa ajili ya masuala hayo ilikuwa ni ndogo.
"Tumekwishaanza
miradi ya ujenzi wa barabara mbalimbali nchi nzima lakini kwa hivi sasa miradi
mingi imesimamishwa kutokana na kuzuiliwa na wananchi wanaodai fidia za maeneo
yao yanayopitishwa barabara na tunasubiri serikali ikamilishe mchakato wa
malipo ili tuweze kuendelea na ujenzi wa barabara hizo" alisema Ngusa.
Kwa upande
wake Ofisa Habari wa TANROADS Aisha Malima amewataka wananchi kutunza
miundombinu ya barabara zilizokwisha kamilika kujengwa ili kuweza kuzifanya
barabara hizo kuwa endelevu na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha kinachotengwa kwa
ajili ya kufanya ukarabati wa barabara hizo.
Alisema kuwa
uharibifu wa miundo mbinu mbalimbali iliyopo kwenye barabara imepelekea
uharibifu wa barabara na kufanya tatizo la msongamano kuwa kubwa katika baadhi
ya maeneo ya nchi hususani katika Jiji la Dar es salaam.
Hata hivyo
Aisha aliwataka madereva na watembea kwa miguu kuzingatia alama zilizowekwa
katika maeneo mbalimbali ya barabara ili kuweza kupunguza uharibifu wa
miubdombinu ya barabara pamoja na kupunguza ajari zinazotokea hapa nchini.
Aliongeza
kuwa katika kukabiliana na tatizo la foleni katika jiji la Dar es salaam
wameanzisha miradi ya ujenzi na upanuzi wa barabara mbalimbali zilizopo baadhi
ya maeneo ili kuweza kupunguza magari mengi kutumia barabara kuu na kupita
katika barabara hizo za pembeni zinazoendelea kujengwa.
No comments:
Post a Comment