Label kubwa ya muziki TZ WCB ambayo iko chini ya msanii mkubwa bongo Diamond Platnumz, ndani yake ikiwasimamia wasanii kama Harmonize, Queen Darling, Raymond na Rich Mavoko.
Akiwa na tweta na waandishi wa habari hivi karibuni mmoja kati ya wasimamizi wa label hiyo Babu Tale amesema wao kama uongozi wa WCB watasimamia na kuhakikisha kuwa wasanii wao watakuwa mfano wa kuigwa katika jamii.
''nikijibu hapo kwenye eneo la nidhamu ni kwamba sisi kama vijana ambao tunaishi na vijana ambao wametoka kwenye familia zao ambazo zina malezi tofauti tofauti, lakini wakija hapa ni lazima wafuate sheria zetu. sitaki kumsifia diamond ni mtu ambae hanna nidhamu ya kuigiza, kwahiyo hawa wengine lazima wafuate tabia ya kaka yao'' alisema Babu Tale.
aliongeza kwa kusema kuwa msanii kwao akitukana kwenye social network (mitandao ya kijamii) au akitukana kwenye stage lazima watamuadhibu.
''kwetu sisi msanii akitukana kwenye social network au akitukana kwenye stage huyo sisi lazima tumuadhibu kuna adhabu ambayo hiyo hatuizingatii kwasababu kila mmoja ana mapenzi yake na wengine wana chuki zao. Adhabu ambayo tatizo linaonekana wazi kwamba hili ni tatizo tunayaita matendo kusudi, kiofisi huwenda akasimamishwa bila jamii kujua, hayo mambo tunafanyia hata sisi viongozi pale tunapokosea''.
No comments:
Post a Comment