![]() |
| Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi |
WAZIRI wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ametoa miezi mitatu kwa watu wote
wanaomiliki Viwanja zaidi ya 1000 kuviendeleza mara moja au kuviuza kwa wananchi kwani kinyume na
hapo hati zao zitafutwa.
Akizungumza jijini Dar es salaam jana katika mkutano uliowakutanisha wataalamu wa kupima na kupanga ardhi kutoka sekta binafsi Lukuvi alisema baadhi ya watu wamekuwa wakimiliki viwanja zaidi ya 1000 huku wakiwa na hati halali lakini walivisajili kwa majina tofauti tofauti jambo ambalo ni kinyume na sheria.
Alisema watu hao wamekuwa wakivihifadhi viwanja hiyo kwa lengo la kuweka akiba ili pale viwanja
vitakapopanda bei waweze kupata faida kubwa.
Waziri lukuvi alisema ndani ya kipindi cha miezi mitatu wamiliki hao wanatakiwa kuviuza viwanja hivyo au kuviendeleza kinyume na hapo wizara hiyo itafuta hati hizo.
Alisema wanaomili viwanja hivyo anawajua na baadhi yao walikuwa wakisaidiwa na watumishi ambao walikuwa sio waaminifu.
"Watu wengi walikuwa wakinunua viwanja vingi na kushidwa kuviendeleza na mwisho wa siku wameishia
kuifadhi hati majumbani kwao jambo ambalo sio nzuri"alisema Waziri Lukuvi.
Alisema serikali aikatazi mtu kumiliki viwanja vingi kinachotakiwa ni kuviendeleza na sio kuviifadhi bila ya kuvifanyia kazi.
Waziri Lukuvi alisema bei za viwanja zinapanda kutokana na baadhi ya watu kuficha viwanja hivyo kwa lengo la kupata faida kubwa.
Alisema lengo la operationi hiyo ni kupunguza kero rasilimali ya ardhi kwa kuhakikisha mwananchi wanapata hati halali za maeneo yaliyopimwa na kupangwa kihalali.
"Serikali imeamua kusajili makampuni 58 ya kupima viwanja na kampuni 33 kwa ajili ya kupanga ili wananchi wapate miliki salama huku ikiendelea kukusanya kodi"alisema Waziri Lukuvi.
Alisema mpango mkakati wa serikali ni kuhakikisha ndani ya mwaka huu hati laki 4 zinamilikiwa na
wananchi walio na viwanja halali .
Katika hatua nyingine Waziri Lukuvi alikabidhi hati 446 kwa wananchi ambao walinyaganywa ardhi
kipindi cha miaka ya nyuma nakusababisha kukata tamaa.
Akikabidhi hati hizo alisema serikali imelenga kuondoa kero ambazo zimekuwa zikisababishwa na migogoro ya ardhi ambayo imekuwa ikisababishwa na manispaa pamoja na wizara.
"Leo nawakabidhi hati hizi za viwanja najua mlikata tamaa kabisa hivyo serikali imeamua kutoa kiwanja katika meeneo ya kigamboni kwa ajili ya fidia na zoezi hili ni endelevu"alisema Waziri.



No comments:
Post a Comment