![]() |
| Viongozi wa Kampuni ya Mult-Choce wakizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uonyeshwaji wa mechi zaidi ya 300 za ligi mbali mbali |
KAMPUNI ya Mult-Choice kupitia king'amuzi chake cha DSTv imepanga kuonyesha mechi zaidi ya 300 kutoka ligi mbali mbali duniani zinazotarajiwa kuanza hivi karibuni.
Hayo yalisemwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Maharage Chande alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akifanya ufunguzi wa kuonyesha mechi za ligi kuu ya Uingereza inayotarajiwa kuanza Jumamosi hii.
"Misimu mipya ya ligi ya bora za soka ulimwenguni imewadia na kuanzia jumamosi hii DSTv kwa uhakika tutaonesha mechi zaid ya 300 ambazo tutaweza kuzitangaza pamoja na kuzifanyia uchambuzi kutoka kwa wachambuzi wetu mahiri ambao wamebobea katika tasnia hii ya mpira wa miguu na hawana mpinzani yeyote hapa barani Afrika," alisema.Alisema kuwa ratiba ya soka barani ulaya imekuwa tofauti na hapo awali ambapo mechi nyingi zilikuwa zikichezwa siku ya jumamosi na jumapili lakini kwa hivi sasa wapenzi wa soka watarajie kupata burudani ya soka kuanzia siku ya ijumaa mpaka jumapili.
Aliongeza kuwa Kampuni hiyo imepanga kuonyesha mechi zote zitakazokuwa zikichezwa katika ligi mbali mbali barani ulaya kwa wateja wake waliolipia kufurushi cha Tsh.84,500 na kwa wale waliolipia kifurushi cha kawaida wataweza kutazama mechi zisizozidi 100.Chande alisema kuwa michuano inayotarajiwa kurushwa na kampuni hiyo ni UEFA Super Cup, Ligi ya Mabingwa ya UEFA, Kombe la FA, Kombe la Capital One, Super Cup ya Hispania, Faunali ya Copa Del Rey, kombe la Ujerumani pamoja na ligi nyinginezo.
Pia Chande alisema kuwa ili kuhakikisha wapenzi wa soka wa DSTv hawakosi tukio lolote lile wamepanga kutoa matangazo ya mechi mbali mbali kwa lugha ya kiswahili pamoja na kupata taarifa kupitia mitandao mbali mbali ambayo imeanzishwa kwa lengo la kutoa taarifa kwao.
"Mashabiki wa Soka wataweza kupata taarifa mbali mbali za soka kupitia tovuti yetu pamoja na program maalum ambazo tunazitumia ili kuweza kujua yale matukio ya papo kwa papo pamoja na matokeo ya mechi kubwa kubwa zitakazokuwa zimechezwa," alisema.



No comments:
Post a Comment