![]() |
| Mmoja kati ya wanajeshi wa kikosi cha zimamoto akijaribu kuwafurumusha Nyuki waliokuwa wamelizingira moja kati ya goli la uwanja huo. |
Mechi moja ya ligi kuu ya kandanda nchini Ecuador iliaahirishwa kwa dharura baada ya nyuki kuvamia uwanjani hapo.
Amini usiamini mechi kati ya River Ecuador na Aucas katika jiji la Guayaquil ilisimamishwa baada ya nyuki waliokuwa wakipaa kutua uwanjani kwa dakika kadhaa na kusababisha hali ya taharuki kwa mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia mpambano kati ya timu hizo mbili.
Wachezaji kadhaa waling'atwa na nyuki huku mashabiki wengi wakijeruhiwa kutokana na kung'atwa na wengine kukanyagana huku wengine wakikanyagana wakati wa kukimbia purukushani hiyo.
Jeshi la zima moto lililazimika kuingilia kati na kujaribu kuwafurumusha wadudu hao waliosababisha taharuki kwa wachezaji na mashabiki.
Mechi hiyo iliyokuwa imechezwa kwa dakika kumi pekee na ilisimamishwa kwa muda wa dakika 30 hivi, hata hivyo refarii aliyekuwa akichezesha mechi hiyo akaamua kuahirisha mechi na kusema kuwa shirikisho la nchi hiyo litapanga tena siku nyingine ya kuweza kurudia kuchezwa kwa mechi hiyo.



No comments:
Post a Comment