Wanasiasa 8 wapandishwa kortini Kenya - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, June 17, 2016

Wanasiasa 8 wapandishwa kortini Kenya


Mahakama ya Kenya
Wanasiawa 8 nchini Kenya kutoka chama tawala na kile cha upinzani, wamefikishwa mahakamani jijini Nairobi baada ya kukaa kororoni kwa muda wa siku tatu kwa makosa ya kutoa matamshi ya uchochezi.

Waendesha mashtaka wamewalaumu kwa kutumia matamshi yanayoweza kusababisha fujo miongoni mwa raia mbali na kudunisha utawala wa taifa.

Video moja iliyowekwa mitandaoni mwishoni mwa juma lililopita, lilimuonyesha mbunge wa chama tawala Jubilee, Moses Kuria, akitoa wito wa kuuawa kwa kinara mkuu wa chama cha upinzani ODM Raila Odinga.

Bwana Kuria amekanusha usemi huo kwa kusema yeye hajawahi kutoa wito kwa mtu yeyote yule kufanya hivyo.

Wabunge wengine wa chama tawala wanaokabiliwa na mashtaka hayo ya uchochezi Ferdinand Waititu (Kabete) and Kimani Ngunjiri (Bahati).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot