Apelekwa Miaka 90 jela kwa kunajisi wanafunzi - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, June 17, 2016

Apelekwa Miaka 90 jela kwa kunajisi wanafunzi


Gari La Mahabusu la Kenya
Mwalimu mmoja wa shule ya msingi katika eneo la kati nchini Kenya amehukumiwa kifungo cha miaka 90 jela kwa kuwanajisi wanafunzi wake.

Hii ni moja kati ya vifungo vya muda mrefu zaidi kuwahi kutolewa kwa watu wanaowaingilia  watoto kinyume na jinsia au wale wenye umri mdogo.

Mwalimu John Gichia Mugi (23) alishtakiwa kwa kuwabaka wavulana 10 wa shule ya msingi ya Muran'ga takriban kilomita 120 magharibi mwa Nairobi mwaka wa 2015.

Mwalimu huyo wa kujitolea atatumikia kifungo cha miaka 10 gerezani mfululizo kwa kila moja ya makosa hayo aliyokutwa na hatia nayo.

Jaji alisema mwalimu alikuwa amesaliti dhamana na imani aliyopewa na wazazi wa wanafunzi hao wachanga ambao alipaswa kuwatunza lakini yeye alifanya kinyume na alivyotakiwa

Wavulana hao walikuwa na ushahidi kuwa Mugi aliwagusa sehemu zao za siri na wakati mwingi anawabusu.

Wakati huo alikuwa akihudumu kama mwalimu anayesimamia maswala ya bweni katika shule yao ya msingi.
Kifungo hicho cha miaka 90 ni ishara tu kuwa sera za serikali ya Kenya imeanza kuchukua hatua kali dhidi ya wale wanaowalawiti watoto nchini humo.

Ikiwa atajaaliwa na maisha marefu, Mugi ataachiliwa akiwa na umri wa miaka 113.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot