Wadau wa Filamu waiasa Serikali - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, June 27, 2016

Wadau wa Filamu waiasa Serikali

Msanii wa Filamu na Balozi wa Watoto waishio katika Mazingira Hatarishi, Salma Jabu(Nisha).
Na Carlos Nichombe.

WADAU wa Tasnia ya Filamu nchini wameitaka Serikali kuweka na kusimamia sera za uwezeshaji kwa jamii ili kuweza kupunguza tatizo la watoto omba omba na wale waishio katika mazingira magumu.

Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Msanii wa Filamu na Balozi wa Watoto waishio katika mazingira hatarishi, Salma Jabu(Nisha) wakati alipokuwa akifuturisha watoto waishio katika mazingira hatarishi iliyofanyika jana katika viwanja vya shule ya sekondari Azania Dar Es Salaam.

Nisha alisema kutokufuatiliwa kwa Sera ya uwezeshaji kwa jamii imepelekea wananchi wengi kuishi katika hali ngumu ya kimaisha na kupelekea watoto kutoroka katika familia na kwenda kutafuta maisha sehemu nyingine ambako hupelekea kuishi katika mazingira magumu.

Nisha akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufuturisha watoto wenye mazingira magumu

"Serikali inabidi isimamie sera waliyoiweka katika kuiwezesha jamii hasa akina mama pamoja na vijana hivyo kwa kusimamia sera hii itaweza kuwapatia wamama wengi mitaji na kuweza kupata kipato kitakacho wasaidia wao na familia zao na kupunguza idadi kubwa ya watoto waishio katika mazingira magumu" alisema Nisha.

Kwa upande wake Shapy Omari(Jk commedian) alisema serikali inapaswa kuwaunga mkono wadau mbali mbali wanaojitokeza katika kupunguza tatizo la watoto wa mitaani ambalo limeonekana kupelekea matatizo mengi kwa watoto hao.

Alisema wapo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya unyanyasaji kwa watoto waishio katika mazingira hatarishi hivyo kuitaka Serikali kupitia Halmashauri za wilaya kutenga maeneo yatakayotumika kulelea watoto hao ili waweze kuepukana na vitendo hivyo wanavyofanyiwa.

"Yapo maeneo mengi hapa nchini ambayo mengine yametelekezwa hivyo ningependa Serikali waweze kuanzisha vituo vya kuwahifadhi watoto waishio katika mazingira magumu ili na wao waweze kupata haki zao kama inavyoelezwa katika haki za binadamu" alisema JK Commedian.

Aidha wananchi waliohudhuria katika hafla hiyo iliyofanyika katika viwanja vya shule ya jangwani waliitaka Serikali kuendelea kutoa elimu ya kujitambua kwa wazazi ili waweze kuwalea watoto wao katika mazingira yatakayokuwa ni sahihi kwao.

Walisema Endapo wazazi watapewa elimu ya kujitambua itakuwa ni vigumu kwao kuweza kuishi pasipo kujishughulisha na kitu chochote kile ambachom kingewainua kiuchumi na kuwafanya waishi kwa Furaha na Familia zao.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot