![]() |
| Ni moja ya vikao vilivyokuwa vikizungumzia maendeleo ya nchi za ulaya |
Na Mwandishi Wetu
Kamishina wa biashara wa umoja wa
ulaya Cecilia Malmström amesema Uingereza inaweza kuanza majadiliano ya
mikataba mipya ya kibiashara iwapo tu itakuwa imejitoa kabisa katika
umoja huo.
"Uhusiano kati yetu na uingereza kwa siku zijazo hautajadiliwa chini ya kifungu cha 50,ambacho ndicho kigezo cha kujitoa.
Hivyo kuna aina mbili tu za majadiliano,moja unajitoa,kisha unajadiliana namna mpya ya uhusiano,au vyovyote inavyokuwa"
Bi.Malmstrom ameongeza kuwa mpaka mikataba hiyo isainiwe ndipo biashara inaweza kufanyika chini ya taasisi ya kimataifa ya kibiashara.



No comments:
Post a Comment