![]() |
| Mwnamuziki wa Zamani Suge Knight |
Na Mwandishi Wetu
Suge Knight amemshtaki mwanamuzki
mwenzake wa R& B Chris Brown mahakamani pamoja na mmiliki wa klabu
moja ya usiku nchini Marekani kufuatia ufyatulianaji wa risasi uliotokea
katika klabu hiyo mwaka 2014.
Kesi hiyo iliyowasilishwa katika mahakama ya Los Angeles inamshtaki Chris Brown na klabu ya West Hollywood Ckub 1 Oak kwa kushindwa kuweka usalama wa kutosha na kumruhusu mtu mmoja aliyejihami kuingia katika kilabu hiyo.
Suge Knight alipigwa risasi tumboni,kifuani na mkono wa kushoto.
Kwa sasa Suge Knight anakabiliwa na kesi ya mauaji baada ya kumgonga mtu na kutoroka.
Inadaiwa kile kilichotokea katika kisa hicho ndio sababu ya yeye kufanya vitendo kama hivyo.
![]() | ||||
| Mwanamuziki Chris Brown |
Wakili wake anasema kuwa alikuwa akijaribu kuwatoroka washambuliaji .




No comments:
Post a Comment