WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Mkazi imepokea msaada wa vifaa vya upimaji ardhi (Total Stations) na mafunzo kwa wafanyakazi wa kitengo cha ardhi kuhusu matumizi yake kutoka kwa wataalamu wa Korea.
Akikaribisha ujumbe wa Wakorea hao Wizarani hapo ulioongozwa na Balozi wa nchi hiyo, Song Geum Young Dar es Salaam juzi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amesema kuwa vifaa hivyo vya upimaji vitasaidia kuhuisha ramani zilizopitwa na wakati na kupunguza migogoro ya ardhi nchini.
Waziri Lukuvi alieleza kuwa idadi ya vifaa vya upimaji vitakavyotolewa vitatunzwa na kumwomba Balozi wa Korea kuangalia uwezekano wa kuongeza idadi ya vifaa hivyo kutoka vinne hadi nane ili visaidie katika maeneo mengi zaidi yanayohitaji kupimwa kutokana na ukumbwa wa nchini hii na kuwataka wataalamu hao kutoka Korea kutoa mafunzo ya matumizi ya vifaa hivyo ikiwamo ndege ya isiyo na rubani (Drone) ya upimaji ramani
Lukuvi alisema Serikali inawashukuru watu wa Korea kwa kutambua umuhimu wa mkakati wa kupima ardhi nchini kwa maendeleo ya Taifa alisema pamoja na vifaa vya upimaji huo pia wameleta ndege isiyo na rubani (Drone) ambayo itatumika kuwapatia mafunzo wapima ramani wa wizara na halmashauri mbalimbali nchini na kumtaka Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani, Justo Lyamuya kuandaa haraka mazingira ya makubaliano ili vifaa hivyo viweze kutumika.
Alisema mafunzo ya matumizi ya ndege na vifaa hivyo yatolewe pia kwa wapima ramani waliopo katika halmashauri na mikoa mbalimbali ili kuwepo na wigo mpana wa ufahamu wa teknolojia hiyo mpya ambayo itarahisisha upimaji na kupunguza gharama kubwa iliyokuwa ikitumika katika ndege za rubani na kuongeza kuwa baada ya mafunzo apewe taarifa ili kujiridhisha kuhusu uwezo wa ndege hizo kabla ya kuzinunua.
Naye Balozi huyo wa Korea alisema nchi yake inajivunia uhusiano mzuri wa kihistoria na Tanzania hivyo itaendelea kutoa msaada ya kiteknolojia kadri inavyohitajika kwa ustawi wa Taifa na kuongeza kuwa ndege moja ya aina hiyo ina uwezo wa kupiga picha 1 kila sekunde na uwezo wa kukaa angani kwa masaa mia 200 mfululizo.
Waziri Lukuvi alishuhudia majaribio ya ndege hiyo ndogo iliyorushwa katika Viwanja vya Gymkhana na kuzunguka maeneo mbalimbali jijini na kurudi bila tatizo majaribio yaliyowavutia wataalamu mbalimbali wa wizara hiyo kutokana na uwezo wa ndege hiyo kujiendesha yenyewe.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Tuesday, June 14, 2016
Tumepokea vifaa vya upimaji ardhi:wizara ya ardhi
Tags
# KITAIFA
About Unknown
Templatesyard is a blogger resources site is a provider of high quality blogger template with premium looking layout and robust design. The main mission of templatesyard is to provide the best quality blogger templates which are professionally designed and perfectlly seo optimized to deliver best result for your blog.
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot


No comments:
Post a Comment