TLP yalaani kitendo cha baadhi ya wapinzani kumbeza Rais - MUANGALIZI

Hot

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, June 14, 2016

TLP yalaani kitendo cha baadhi ya wapinzani kumbeza Rais


Mwenyekiti wa Chama cha TLP Dkt. Agugostino Lyatonga Mrema,(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani Dar es Salaam jana, kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea nchini,(kulia) ni Katibu Mkuu wa chama hicho,Nancy Mrikaria.

SEKRETERIETI ya Chama Cha Tanzania Labour(TLP), kimelaani vikali kitendo cha baadhi ya wapinzani kumshutumu Rais John Magufuli kuwa ,anakiuka haki za binadamu, anawaonea, anaua Demokrasia, pamoja na kuvunja  sheria na katiba wakati wenyewe ndio vinara wakubwa wa kufanya  vitendo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana Mwenyekiti wa chama hicho Augustino Mrema alisema kuwa kitendo hicho kilicho fanywa na baadhi ya wapinzani ni kinyumne na mshikamano kati ya vyama vya upinzani,jambo ambalo linasababisha chama tawala kuendelea kuwa na wabunge wengi bungeni.

Pia Sekreterieti hiyo inalaani baadhi ya vyama vya Siasa kutumia nyumba za ibada kama vichaka vya kuendeshea kampeni chafu kipindi cha uchaguzi dhidi ya wapinzani wenzao na kuwatumia baadhi ya viongozi wa dini kuwaangamiza baadhi ya wapinzani wenzao kama walivyo fanya katika jimbo la vunjo.

"Kitendo kinacho fanywa na baadhi vyama vya wapinzani kuwatumia viongozi wa dini kuwa mawakala katika jimbo la vunjo ndicho kilipelekea hadi nikapoteza jimbo langu,mfano mzuri ni katika mkutano wa UKAWA wa Septemba 27 mwaka jana uliofanyika katika viwanja vya polisi na Himo ulionyesha dhahiri kumnadi mpinzani wangu Jemsi Mbatia"alisema Mrema

Hatahivyo Sekreterieti imesikitishwa na Kitendo kilichofanywa na baadhi ya vyama vya upinzani na kuyaacha majimbo mengine yaliyokuwa ya upinzani na kuyaacha yakichukuliwa na Chama tawala.
Pia alisema kuwa ni kwanini nguvu hizo zilizo tumika katika jimbo la vunjo kuing'oa TLP isingetumika katika kulinda majimbo mengine yaliyo kuwa ya upinzani au kuongeza idadi ya wabunge wa upinzani bungeni.

"Hizo zilikuwa hujuma za kiiuwa TLP kisiasa na kusababisha chama kukosa ubunge nguvu zote zilizo elekezwa vunjo zingeweza kusaidia kulinda majimbo mengine ya upinzani na kuongeza idadi ya wapinzani bungeni"alisema

Aidha Sekreterieti hiyo imelilaumu Jeshi la polisi Mkoa wa Kilimanjaro kwa kutowafikisha Mahakamani watuhumiwa  waliokamatwa na karatasi zilizo ghushiwa na kusambazwa kwa lengo la kumhujumu Mwenyekiti wao wa taifa.

Pia Sekreterieti hiyo imeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC,kupitia upya Sheria na kanuni za Uchaguzi ili kutoa adhabu kali na ikiwezekana kuwaondowa  katika Uchaguzi, wagombea wote watakao kiuka Sheria na kanuni za Uchaguzi,badala ya kutoa onyo pekee.

Aidha aliongeza kuwa anamwomba Rais Magufuli aunde kamati ili kuchunguza uhalali wa nani angetakiwa kuwa mbunge jimbo hilo kwani hata msimamizi wa uchaguzi alibaini kuwa TLP ilichezewa rafu lakini alipo fungua kesi mahakamani walimchangia kama mpira wa kona na kumlazimisha atoe milioni 40 kama garama ya kuendeshea kesi hiyo.







 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot