![]() |
| Baadhi ya wachezaji wa timu ya Serengeti boys wakishangilia ushindi walioupata latika mchezo wao dhidi ya sheli sheli uliopigwa wikiendi hii. |
Na Carlos Nichombe
TIMU ya soka ya taifa ya vijana wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys leo imejiweka kwenye nafasi
nzuri ya kufuzu kucheza fainali za kombe Afrika baada ya kuichapa Sheli Sheli bao 3-0 katika mechi
iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mabao hayo ya Serengeti Boys yalifungwa na Nickson Kibabage'16' Ibrahim Abdallah '22' pamoja na
mlinzi wa kati Ally Hussein '61' ambaye alifunga goli hilo kwa mkwaju wa penalti mara baada ya
mchezaji wa timu ya sheli sheli kuunawa mpira huo katika eneo la 18.
Kwa Ushindi huo Serengeti Boys watakuwa na kazi nyepesi katika mchezo wa marudiano utakaopigwa
wiki ijayo huko Sheli Sheli ambako itahitaji suluhu ya bila bila au hata ya kufungana na kuweza kufanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo.
Waamuzi wanne kutoka Ethiopia, ndio waliochezesha mchezo huo. Waamuzi hao ni Belay Asserese ambaye
ni mwamuzi wa kati wakati wasaidizi wake ni Tigle Belachew upande wa kulia na Kinfe Yilma upande wa
kushoto huku mwamuzi wa akiba atakuwa Lemma Nigussie pamoja na Kamishna wa mchezo huo atakuwa
ni Bester Kalombo.
Mchezo huo ulikuwa ni mzuri kwa timu ya Serengeti boys kwa kuwa wao ndio walio kuwa wakiutawala
mpira huo kuliko washindani wao wa timu ya sheli sheli ambako Serengeti Boys walitawala mpira huo
kwa asilimia 60 na wapinzani wao kwa asilimia 40.
Kwa Upande wake kocha mkuu wa Timu ya Serengeti Boys Bakari Shime amesema kuwa kilichofanywa leo ni mwanzo wa safari yao ya kuelekea katika mafanikio.
aliongeza kuwa anaiandaa timu yake vyema ili waweze kwenda kupata ushindi mwingine wa kishindo
utakao wapa tiketi ya kuweza kuendelea mbele katika michuano hiyo.
"Safari yetu haitokiwa rahisi sana lakini tunaamini tutaweza kupita katika hatua hiyo iliyopo mbele yetu kwa hiyo niwaombe Watanzania wazidi kutuamini kwamba tunaweza na tutafanya kweli" alisema Shime.



No comments:
Post a Comment